Naomba ushauri: Nimeondoka kwa wazazi kisa wamekataa kuniendeleza chuo. Nimekuja Lindi kufanya kibarua

Naomba ushauri: Nimeondoka kwa wazazi kisa wamekataa kuniendeleza chuo. Nimekuja Lindi kufanya kibarua

Joined
Jan 26, 2019
Posts
87
Reaction score
113
Habari wanajukwaa natumai wazima,

Jamani mimi nina umri( 26) nina elimu ya form six. Nimeamua kutimuka nyumbani kabisa kisa mzee mtata kweli kakataa kuniendeleza chuo na pia hataki nitafute vya kujitegemea kwa sasa nimeamua kuenda kwenye miji ya huku LINDI sina chochote nategemea kuanza vibarua kuvuna alizeti na mtama.

Lengo langu nikitegeshea kipindi cha mvua ni Lime zao la UFUTA niuze nipatae kimtaji. Kwa wale wazoefu JE NIPO SAHIHI KATIKA KUJITAFUTIA AU NITATENGENEZA CHUKI KWA WAZAZI.
 
Uvune miezi hii halafu utunze pesa mpaka msimu wa kilimo,kwanza huko kwenye vibarua utapata pesa ya kula tu Lindi hakuna mkulima mkubwa kwamba utapata pesa ya maana.fundisha tution
 
Uvune miezi hii halafu utunze pesa mpaka msimu wa kilimo,kwanza huko kwenye vibarua utapata pesa ya kula tu Lindi hakuna mkulima mkubwa kwamba utapata pesa ya maana.fundisha tution
Natunza kwa mfumo wa kununua kuku afu nawaacha mpaka kilimo
 
Lindi uko sehemu gani boss
Nakushauri kwa Sasa nenda vijiji vifutavyo katafute mtaji wa kulima mwezi December kwani kipindi hiki Cha msimu wa korosho
1.NAMIYOMIYO MASASI VIJIJINI HUKO
2.NANYAMBA MTWARA VIJIJINI
UKIPATA MTAJI
RUDI WILAYA YA RUANGWA VIJIJINI
NENDA
1.NANJILINJI KAPIGE UFUTA utanishukuru
 
Mkuu mimi nipo kilwa kijiji kimoja kinaitwa ZINGA barabara ya kuelekea Liwale nipo kwenye miji ya wasukuma naunga unga kwani wewe upo wapi mkuu
 
Mkuu mimi nipo kilwa kijiji kimoja kinaitwa ZINGA barabara ya kuelekea Liwale nipo kwenye miji ya wasukuma naunga unga kwani wewe upo wapi mkuu
Kiongoz mm Ni mzaliwa wa kusini
Ila kwa Sasa Niko mkoa wa songwe
Fanya hivyo kiongoz,
 
Back
Top Bottom