Naomba ushauri, nimezoea kuendesha automatic sasa juzi nimepata manual Vitz

Mkuu kama moja inazima basi mbili ndiyo huiwezi kabisa japo tafuti ni ndogo na wengi hutumia mbili kuondokea, shida hapo ni wewe jinsi ya kubalance clutch na mafuta
Nimekuelewa mkuu. Nishaanza kufanyia mazoezi. Naona matokeo mazuri
 
Usikute clutch yake ndiyo zile unaachia mpaka goti linafika kidevuni
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umetisha sana.
 
Ni kweli.
Driving school unafundishwa manual kwa kutumia liCruiser flani after 3/4 weeks ukimaliza ukirudi street unaaendesha auto maana ndio inayopatikana. Sasa kwa muda wote huo kumbukumbu za manual zinapotea.

Kuna aliwahi kufananisha udereva wa auto kama kucheza game la magari (Fast Motor GP) kwenye simu. Mradi ujue kunyoosha na kuongeza mafuta[emoji23][emoji23]
 
Hii Maelezo murua lakini pia
Akisimama kwenye foleni arudishe gia hadi moja inafanya wakarti wa kuondoka isiwe raisi kuzima. kwa sehemu tambarare anaweza kurudisha nakuanzia gia #2 ila kwa kuwa anajifunza awe anarudisha hadi moja....gari haita zima kwa urahisi ila muhimu pia aanze kukanyaga mafuta taratibu; akikanyaga mafuta meeti iweza kuzima pia...
 
Ndio mana huwa nashangaa wanaoponda wasiojua manual wakati gari za manual haizipatikani...
Hata wazungu huko wameacha kutoa gari za manual labda uweke speciail oder
 
Ndio mana huwa nashangaa wanaoponda wasiojua manual wakati gari za manual haizipatikani...
Hata wazungu huko wameacha kutoa gari za manual labda uweke speciail oder
Sahivi kuna gari zinajiendesha zenyewe.

Miaka 10 ijayo watu watakuwa wanakaa kwenye gari linatembea lenyewe.
 
Ndio mana huwa nashangaa wanaoponda wasiojua manual wakati gari za manual haizipatikani...
Hata wazungu huko wameacha kutoa gari za manual labda uweke speciail oder
Hapo UK tu gari za Manual ni nyingi kuliko auto.

Na kwa UK anayejua manual then leseni yake inamruhusu kuendesha na auto,lkn mwenye kujua auto na manual hajui then leseni yake haitamruhusu kuendesha gari manual mpk akafanye driving test na atahitajika ku-upgrade leseni yake.
 
Angalia gari za matoleo ya 2017 kuja juu nying zimetoka automatic ni suala pa mda tu manual zitabaki za kujifunzia driving
 
Ukishazoea inakua kawaida sana. Na utaenjoy Sana. Ukija kuendesha auto unakua bored
 
Shida sio clutch au shida ya gari ya fundi. With manual transmissions kuondoka huwa ni issue:-
1. Always ondoka na gear number moja. Kwenye round about/mwendo mdogo tumia Namba 2.
2. Wakati wa kutoka weka moto kidogo kidogo huku unaachia clutch taratibu huku ukisikilizia na muunguramo wa gari usiachie kabisa mpaka gari tutembee.
3. Fanya practices baada ya muda utakaa Sawa.
 
Angalia gari za matoleo ya 2017 kuja juu nying zimetoka automatic ni suala pa mda tu manual zitabaki za kujifunzia driving
Mkuu, international companies wananunua manual transmission mara nyingi.

Ofisini kwetu magari yote ni manual na yote YOM ni between 2018 - 2020.
Na hii ni company policy worldwide.

Wote walio kwenye position ya kuwa na gari ya ofisi lazima ujue tu manual.
 
Hii scenario imenikuta sana pale kwenye kamwinuko pale kutoka rafia kuelekea tegeta kwenye mataa ya mbuyuni. Kelele nlizopigiwa pale mpaka nikazima gari na kuwasha hazard.

Hapo kwenye kuswitch clutch na mafuta ndio panapochanganya yaan
Hiki ndio kipengele cha manual tu, sijaweza hapo tu ndio maana manual siijui mpaka sasa natamani kwenda NIT ila pale naskia wanakupa eicher uhangaike nalo ukizengua unaanza upya
 
Sio UK to hata Denmark wanatumia gari za manual sana. Hata gari inayotoka 2021 unakuta ni Manual Tranny 😸!
Dream yangu ni kuwa na Land Cruiser la Manual nyumbani kwangu kama Gari ya mzee 😹😹😹 madogo najua hawatagusa.
 
Hiki ndio kipengele cha manual tu, sijaweza hapo tu ndio maana manual siijui mpaka sasa natamani kwenda NIT ila pale naskia wanakupa eicher uhangaike nalo ukizengua unaanza upya
Kama una experience ya ku drive an automatic car,kujifunza manual ni kitu kidogo sana believe me.Challenge kubwa ya Manual mara nyingi ni kwenye kuondoka na kusimama otherwise ukiwa kwenye motion haina difference yoyote ya maana na Automatic trans.Just believe yourself-& Nothing special.
 
Nakubali
 
Kuendesha manual kwenye safari ndefu sio shida ila kwahapa town asee ni shida sana. Mkono hautulii kila saa unashuka na kupanda gia na usiombe upate kilima halafu kuna folen hesabu yake ni ya hali ya juu sana.
 
Naamini hilo sababu ndio kinachonitatiza mpaka sasa!
 
Nimecheka sana na comment za wadau, anyway manual ni kati ya gari nzuri sana na hata ukiendesha unahisi kabisa uko engaged na gari yako, binafsi sijaenda driving school hata kwa bahata mbaya ila nilijifunza auto na manual kupitia youtube na hadi sasa naendesha manual na wala sifikirii kuiacha.

Ukiwa kwenye foleni isiyotembea kwa muda huna haja ya kuchosha mguu kwa kukanyaga clutch weka tu neutral kanyaga zako break tu au piga zako hata hand break then relax, na ukiona foleni imeanza kutembea weka gear No. 1 (gear No. 2 sikushauri hasa kwa uwezo wa engine ya gari yako maana utaichosha clutch mapema). Then ukishaweka zako 1 anza kuachia clutch taratibu huku unaisikilizia gari ukiona imeanza kumove taratibu au mlio unabadilika, anza kuongeza mafuta kidogo kidogo, tena kama ni zile foleni za kusogea hatua mbili ukiweza kubalance clutch yako vizuri wala hutakuwa na haja ya kukanya mafuta maana usipokuwa makini kwenye mafuta unaweza ukabutua gari ya mbele yako.
 
Kweli kabisa asilimia kubwa ni manual mkuu unafahamu UK.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…