Itoye
JF-Expert Member
- Sep 29, 2017
- 531
- 1,023
Wakuu salaam.
Kuanzia mwezi February 2017 nilianza ufugaji wa kuku wa mayai, kwa fedha ndogo ya akiba niliyokua nayo na nilifanikiwa kuanza na kuku 300, kutokana na ugeni ktk eneo hili na hadi sasa wapo takribani kuku wasiozidi 200.
Kwa kipindi hiki chote ambacho binafsi kimekua ni kipindi cha kujifunza nimepata uzoefu na elimu nzuri tu juu ya ufugaji. Kutokana na elimu na uzoefu huu mdogo nilioupata nimeona ni wakati muafaka wa kukuza mradi huu ili pia kuongeza na kipato.
Malengo niliyonayo na kwa mazingira niliyopo nataka kufuga kuku 1000 wa mayai, ambao kwa makisio niliyopiga kwa kipindi chote tangia wakiwa vifaranga hadi watakapofikia umri wa kuanza kutaga nitahitaji kati ya Tsh 9,000,000/- hadi Tsh 10,000,000/- hii ikijuimuisha gharama ya chakula na marekebisho kidogo ya mabanda (nafugia DSM) na hadi sasa nina kiasi cha Tsh 2,000,000/- pungufu ya Tsh 8,000,000/-.
Natambua JF kuna watu wenye ujuzi na uzoefu mkubwa kwenye eneo hili na naamini pia wapo ambao kuna wakati walikuwa kwenye situation kama hii na wakafanikiwa, naomba kupata ushauri ni njia zipi nitumie au nini nifanye ili nipate kiasi cha fedha nilichopungukiwa ili hatimaye niweze kuuendeleza mradi wangu na kufikia malengo niliyonayo.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushauri nitakaoupata.
Asanteni.
Sent using Jamii Forums mobile app