Naomba ushauri. Nna tatizo serious

Naomba ushauri. Nna tatizo serious

Annonymous

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2013
Posts
688
Reaction score
1,126
Mm n kijana wa 28yrs. Ilitokea kupata watoto wawili wa kike na binti wa kichaga (muuru) ambapo watoto hao wote walikuwa prematured chini ya miezi 7na walikufa wote kwa nyakati tofauti (walipishana mwaka moja).

Mtoto wa wanza alikuwa prematured wa miezi6 hospital ilikataa kumtoa ingawa ilituonesha amefariki kwa madai wanamfanyia uchunguzi zaidi, wapili prematured wa miezi 7 tulimchukua kumzikia ardhi ya hyo binti. Wote walikuwa wa kike.

Baada ya hayo yote maisha yalisonga kawaida mpaka ikatokea ugomv wa mm na hyo binti ambao kimsingi ulianzishwa na dadaake hyo binti. Baadae dadake alimshuri arudi nyumbani kwao waende mwanza nayeye akakubali na akarudi kwao kwakaenda mwanza. Nikaambiwa nisikanyage kwao na hata kwenda kuangalia kaburi la huyo mtoto.

Tatizo: Toka huyo binti alipoondoka kila usiku kabla sijalala au nnapokuwa nmetulia tu taswira ya hyo mtoto akiwa monchwari au ndani ya incubator au ya siku ya mazishi yake (msiba wake) huwa inarudi kichwani

Naomba ushauri nifanyeje mana kuna wakati akili inastak na kichwa kinakuwa kizito na hakiwazi lolote zaidi ya hyo taswira mpk iishe ndio akili inaanza kuwaza kawaida na mood inarudi normal

Naomba ushauri nifanyeje
 
kwa uelewa wangu mdogo,naona ujiepushe na mazingira ya kukaa peke ako peke ako,fanya ibada kwa wingi utasahau tu jipe muda...ya utaalam zaidi subir wajuvi wa mambo wanakuja!
 
Damu nzito kuliko maji. Hakuna namna utaachana na hali hiyo usipokuwa mtu wa sala sana. Ukiwa mtu wa kuomba itakusaidia kuamini kuwa ipo siku utamuona tena. Na binadamu wote njia yao ni moja. Mungu hutoa faraja ya kweli na kusahau kwasababu wewe sio wa kwanza kufiwa.
 
Tatizo lako unaweza kushauriwa kiutaalamu au kiimani.kwa sababu mmeshaachana na mwenzio,kinachofuata ni kila mmoja apambane na maisha yake.Kwa sasa jaribu kujiepusha na mazingira ya upweke tafuta mtu au ndugu yako muishi naye kwa muda wakati ukipitia katika hiyo hali.
 
Pole sana...

ULishuhudia vitu ambavyi akili yao haijazoea... kama unaishi peke yako tafuta mtu ukae nae...


Cc: mahondaw
 
Ukianza kuweka mambo ya imani na Mungu, nakwambia utakwama, nakwambia tena utakwama.
Kama walivyosema hapo juu wadau, epuka kukaa kipekee pekee, jichanganye.
 
Siwezi kushauri kwasababu ulitaja kabila la mke ili kurahisisha majibu ya wachangiaji
 
Back
Top Bottom