Mwana Mpotevu
Platinum Member
- Sep 7, 2011
- 3,295
- 2,501
Wanajamvi
Nilikuwa na Mpenzi wangu ambaye tumekuwa katika mapenzi kwa muda mrefu sanaa, ni karibu miaka sita. katikati ya uhusiano wetu alipata ujauzito na tuna mtoto mmoja ana miaka minne lakini hatujaoana. kuanzia mwaka jana tabia za huyo mpenzi wangu zimekuwa zikibadilika sana na inaonekana kama amekuwa na kiburi kwa kiasi kikubwa na hakuna tena mapenzi kama zamani. Kutokana na hali hiyo na jitihada za kuokoa penzi letu ninavyoona linazidi kwenda kombo, nimeamua kuanzisha uhusiano na dada mwingine ili ikiwezekana nije nifunge naye ndoa huku nikiangalia mwelekeo wa yule wa kwanza pia kama atabadilika na kurejea kwenye mstari kama zamani au la.
Uhusiano wangu mpya una kama mwaka mmoja kasoro, Nilimwambia ukweli huyu mpenzi wangu mpya kwamba nina mtoto toka kwa mpenzi wangu wa awali ambaye naona kama mahusiano yanakwenda kombo. Kwahiyo tumeingia katika mapenzi huku akijua kuwa nina mtoto mmoja na yeye akaniambia ana mtoto mmoja alizaa miaka sita iliyopita na mtoto huyo anaishi na dadake kwa sasa.
Katika siku za hivi karibuni, huyu mpenzi wangu mpya amefanya kitu ambacho ndio kimenisukuma kuomba ushauri hapa jamvini. Amemuandikia mpenzi wangu wa awali ujumbe kwenye FB (inbox) akimwambia kuhusu mimi kuwa na uhusiano na mdada mwingine (hakutaka kujitaja kwamba ni yeye lakini description alizozitaja za huyo mdada ni wazi alikuwa anajitaja yeye mwenyewe). Na mbaya zaidi amemwambia mambo mengi kuhusu mimi na yeye na pia amemwambia namna (huyo mpenzi wangu mpya) alivyokuja kwangu na vitu alivyovikuta na hata ramani ya vyumba vyangu ilivyo huku akidai kahadithiwa na mpenzi wangu mpya yote hayo (lakini ukweli ni yeye mwenyewe mwandishi wa msg ndie huyo mpenzi wangu mpya).
Mwisho akamshauri eti aachane kabisa na mimi maana sitaweza kumsaidia lolote katika masiaha yake na aangalie maisha mapya. Mimi nilionyeshwa kwa macho yangu hiyo msg na gf wangu wa mwanzo na jinsi ilivyoandikwa sikuwa na shaka nikajua fika kuwa aliyeandika ni yuleyule mpenzi wangu mpya maana ameandika mambo ya ndani sanaaaaa ambayo si rahisi mtu zaidi ya sie wawili kujua.
Nilipojaribu kumuuliza yule mpenzi wangu mpya kuhusu ujumbe ule, akakana na kusema kuna siku alikutana na rafiki yake mmoja akamdokeza kuhusu uhusiano wetu, na akasema huenda huyo rafiki yake ndio aliyeandika hayo yote na akawa akijiapiza kuwa huyo rafiki yake eti anataka kusababisha uhusiano wetu mimi na yeye ufe. Nashindwa kuamini sana kwa jinsi mambo yaliyo kwenye ule ujumbe yanavyoeleza maana ni mambo ya ndani sana kiasi kwamba sio rahisi kwa mtu kumwabia rafiki yake mambo hayo.
Najikuta nimechanganyikiwa nini lengo la huyu mpenzi wangu mpya kuandika jambo kama lile kwa mpenzi wangu wa zamani. Sijawahi kumdokeza kwamba nataka kumuoa lakini tumekuwa katika mapenzi muda sasa na ukweli natafuta mtu wa uhakika nitayetaka kumuoa. Naomba ushauri wenu huyu mtu wa pili ananifaa kweli na nini lengo lake kuandika mambo yetu kwa mpenzi wangu wa zamani??
Naombeni msinishambulie kwa kuwa na wapenzi wawili maana nimewapa scenario iliyonifanya niingie katika uhusiano na huyu wa pili baada ya yule wa kkwanza kubadilika kitabia, sasa huyu wa pili naye ananichanganya nashindwa kumuelewa sasa.