Naomba ushauri wa dawa za palizi kwenye shamba la ufuta

Naomba ushauri wa dawa za palizi kwenye shamba la ufuta

Mandison

Senior Member
Joined
Mar 10, 2017
Posts
191
Reaction score
110
Habari wana JF!

Naombeni ushauri au uzoefu wenu kuhusu madawa yanayoweza kutumika kufanya palizi kwenye shamba la ufuta.

Nafahamu yapo madawa ya kufanya palizi kwenye mpunga na hata mahindi na kwa kiasi kikubwa yanasaidia kupunguza gharama za kilimo kwa wanaolima mashamba makubwa.

Nimejaribu kutafuta madawa ya palizi ya ufuta lakini bado sijafanikiwa. Naomba ambaye anafahamu hayo madawa kama yapo anielekeze tafadhali.
 
Ufuta, Karanga, na mazao mengine yanayofanana na hayo hayana viuagugu! Kwasababu dawa zinazotengenezwa zina ua majani yenye asili ya majani mapana ambayo ufuta na karanga vimo kwenye kundi hilo.
 
Back
Top Bottom