Naomba ushauri wa hekima kwa hili.

ANTA

Member
Joined
Nov 20, 2011
Posts
66
Reaction score
7
Ni mazingira gani, au ni umri gani mwanaume anafikia hatua anaamua
kutokuoa kabisa. Nalizimishwa kuoa na ndugu, jamaa na marafiki, (sijui nimuoe nani sasa) eti umri nilionao (32) ndo wa kufanya
maamuzi, baada ya hapo eti nitaona ni kawaida tu kuishi bila mke au nitakuwa naona mke ni kero tu, mchumba wangu anasoma chuo, bado miaka 2 amalize. Kwao hawakubali kabisa nimuoe mpaka amalize kusoma, nami nakubaliana nao. Na tatizo kubwa, nina ndugu zangu watatu na wakubwa zaidi yangu (35,39,39), wana maisha yao ya Mtanzania wa kawaida. Lakini hawajaoa na hawataki tena mtu awashauri kuoa, wakisema kukaa na kuanza kubanwa na mke ni kero kwao. Je, ni kweli ukipita umri fulani hamu na hamasa ya kuwa na mke inapungua au inapotea kabisa. kweli nahitaji kukaa na mke, ila wadadisi wanasema kuna muda unafika hamu inaisha.

Mada hii imetugawa usiku wa jana na jamaa zangu. nimeamua kuileta kupata ushauri wa kitaalamu, kimazoea na kimazingira.
Ahsante sana.
 
katika kila rule kuna exceptions.

Kuoa inategemea kama umepata right patina, huoi kama fasheni kufurahisha baraza, unaoa sababu unasikia msukumo binafsi ya kuoa.
Na msukumo unaupata ukipata right patina.

Hata kama una miaka 70, ukikutana na right patina utaoa tu.
 
usikubali kuendeshwa na akili za watu, ww ni mtu mzima una maamuzi yako binafsi ,na kuhusu swala la kuoa kama unamchumba msubirie amalize muoane kwani ukiforce kumuoa mtu mwingine kisa kukidhi haja za ndugu zako utaumia sana. na ukumbuke . mali na uridhi mtu uridthi kwa babaye ila mke mwema hutoka kwa Bwana,ninakushauri ukae na mungu wako vizuri akusidie .pia ndoa ni agano ambalo mungu ameweka na alisisitiza akasema si vema mtu huyu akae peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanana nae ,hivyo ni vizuri uwe na ndoa kwasababu mungu alijua ww kama ww hautaweza ,bila hivyo utaishia kwenye maisha ya dhambi tu na anasa.kingine kuhusu hao ndugu zako inaonekana kwenye familia yenu au koo zenu kuna tatizo la kutokuoa ,hivyo unatakiwa ww kama ww usimamie hilo.Asante!
 
Hizo mambo za kuoa bro sio za kukimbilia, watapiga vigelegele mwisho wa siku wanakuacha wewe na mwenzako mnaanza safari ngumu. Kama hujisikii kuoa subiri kwanza kuna wakati tu utafika akili yako itakutuma uwe na mwenzako. Mwengine hiyo akili huja miaka 25, mwengine 35 , mwengine 40 wala usifanye papara.
 
Sijasikia watu wanaoa kwa kufurahisha baraza hii kali aisay.
 
nadhani kabla ya kuoa lazima uwe na mahusiano na mhusika au mtu yoyote , jipime kwanza katika mahusiano yako yakoje na huyo uliye nae, pia kuna suala la utayari wewe kama wewe unaonaje uko tayari kuanzisha familia? maana kuoa si suala la kuishi na mwenza kumbuka kuna matunda ya ndoa ambayo ni watoto
 
roho wa bwana akupe maamuz,uclazmishe km hujiskii kwa sasa,eti sababu ya kuwaridhisha ndugu.
 
Oa ukiwa ready lakini hiyo habari kuna ukweli fulani utaona kero mke sababu ushazoea uhuru wako wa kufanya kila kitu kipekee. Jengine wanataka kukuepusha na dhambi za uzinzi, wewe waeleze kuwa kuna mtu unamsubiri mara amalizapo chuo mtayaweka mambo swawa.
 
achana nao haiwezekan wakulazmishe kuoa wana lao jambo. tafakari
 
Hekima ni nini? We huna?
hekima ninayo. maana siwezi kutoa ushauri kama ulionipa kwa mtu aliyeniomba ushauri. ndo maana nilisema ushauri wa hekima, basi wewe hukusitahili kutoa ashauri, maana huna hekima. nitumie nafasi hii kuwashukuru walionipa ushauri.
 
Dahhh
sijui kama huo utafiti una ukweli ndani yake..

Usema ukweli mambo ya ndoa ni ya wawili tu ..
Hao ndugu zako wala hata wasiku harakishe ..
Kwa vile tayari unamchumba na unamsubiri tu
amalize shule .. Basi we fanya hivyo ..

32 Kwa kijana bado mdogo sana..
Fanya utakalo ilimradi uwe na furaha na si kuwafurahisha wengine..
 
Asikulazimishe mtu kuoa usiyempenda hata kama ni Wazazi wako. Msubiri huyo umpendaye amalize masomo ili mfunge pingu za maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…