Naomba ushauri wa kibiashara, nina mtaji wa Tsh 50,000

Naomba ushauri wa kibiashara, nina mtaji wa Tsh 50,000

Kama uko dar es salaam tafuta sehemu pembezoni mwa barabara uuze matunda unaweza kuanza na machungwa pamoja na matikiti na mananasi ya vipande.
 
Biashara ya genge vitu vinaharibika muda wowote Mimi ushauri Kama ananguvu na afya njema angeaza na biashara ya uchinga ata wakuuza vyombo vijiko,sahani nguo za ndani,radio nk kwa mtaji wake anaweza kuingiza hata 10k kwa siku akienda miezi miwili hivi atakuwa amepata mtaji wa laki tatu

Laki tatu sasa inatosha kabisa kuanzisha duka genge
 
chemsha mihogo, chemsha chachandu, tia kwenye hotpot, beba na maji ya kunawia mikono.

Jisogeze maeneo ya viwanja vya shule mida ya kutoka mapumziko.
 
Naombeni USHAURI WA kibiashara wakuu; nina mtaji WA Tsh 50,000/=(Elf hamsin). Je, Kwa mji WA Kilosa, nianzishe biashara Gani?

Ahsanten sana!

Mtaji mkubwa sana huo.


Nunua mafuta ya kuoikia lita tatu, nunua unga wa ngano kilo nne, nunua maharage kilo mbili, nadhani frying pan unayo na kisumumio, nunua mkaa debe moja, kisha anza biashara ya kutengeneza chapati na maharage na kama utapenda weka na chai ya tangawizi.

Baada ya miezi mitano utakuwa na wateja wengi Saba hasa ukiwa msafi.... utakuja kutoa ushuhuda hapa


Cha muhimu kuwa na nidhamu ya pesa na vyakula vikibaki ndio chakula chako.

Kila la heri
 
Naombeni USHAURI WA kibiashara wakuu; nina mtaji WA Tsh 50,000/=(Elf hamsin). Je, Kwa mji WA Kilosa, nianzishe biashara Gani?

Ahsanten sana!
Nunua mayai trei mbili kilo moja 8000 uza stend hapa aibu weke pembeni chemsa uza yai moja 500 mayai yakiisha utakuwa faida 7000 kwa trei zote mbili 14000
Uza kama mwezi hiii kila siku hakikisha unaauza trei mbili mwisho mwezi faida nzima itakuwa 420000tsh umekosa kabisa laki tatu kami.....

Uza hivyo miezi miwili utakuwa na laki nane
Hama kilosa njoo dar sasa na laki nane kwenye mpesa ......ukifika
Nenda mabibo nunua matunda ya laki mbili azima na torori anza kutembeze mitaani au stend pembeni basi hata uzauza utapata mtaji kama million 6 hivi ukiwa na bidiii

Sasa fungua genge la matunda mtaa uliochangamka kisha hela zingine chukua boda boda ya mkopo pale kampuni ya WATU mchana unauza matunda usiku BOLT boda boda hadi sasa saba usiku fanya hivi miezi 7 utapata million 15 faida za bolt kila siku 40000 bado genge hapo lazima million 15 upate


basi unanitafuta nikuelekeze biasha ya kuuza vifaa vya simu kutoka china na jinsi ya kuagiza uwe tajiri kama mimi sawa kijana .

Safari njema kwenye stage ya kwanza ya mayai ....tukutane stage ya mwisho ukiwa na million 15....
 
Inategemeana sehemu alipo kwa dar angeanza biashara ya kuuza kahawa na kashati kama ni mikoani angeuza vitu vidogo vidogo vya kutembeza kama sufuria na sahani na vikombe
 
Back
Top Bottom