Naomba ushauri wa kisheria juu ya swala hili

Llio 002

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Posts
1,636
Reaction score
2,053
habari wana jf, kuna kesi nimeisikia mahakama flani hivi ikiwahusisha mchimba kisima na mteja wake sasa mteja alimpa kazi ya kuchimba kisima jamaa huyo katika makubaliano walikubaliana kuwa kisima kitaghalimu shillingi millioni kumi maana ni kisima cha mita 150 na katika makubaliano yao ya mdomo walikubaliana kuwa anatakiwa alipe asilimia 80 kama advance wakifika saiti siku ya kwanza na asilimia 20 italipwa pale watakapohitaji kununua mabomba (pvc) kwa ajili ya kuyaweka ndani ya kisima.

Siku waliyofika saiti jamaa alilipwa millioni 2 na nusu kama advance ambapo ni nje ya makubaliano lakini akakubali akaja akalipwa millioni tano na nusu siku 2 baadaye jumla ikawa ni millioni 8 hapo akawakatia risiti inayoonyesha kuwa amelipwa shillingi millioni 8 lakini bado anadai millioni 2. Jamaa wakaendelea na kazi yao ya uchimbaji walipofikia mita 140 fundi akampigia bosi mwenye kisima chake akamwambia kuwa sasa wamebakiza mita 10 kumaliza kuchimba ili kesho waanze hatua nyingine ambayo sio ngumu ni rahisi tu hatua yenyewe ni kulimu shimo ( kulitanua shimo na kulifanya softy ) ambapo kazi hiyo kwa kisima cha mita 150 inafanyika ndani ya muda mchache tu kama mkianza saa 2 mpaka saa nane watakuwa tayari wameshamaliza hapo itabidi waweke mabomba ( Pvc ) kwa hiyo atatakiwa hiyo kesho aziwasilishe zile hela zilizo baki 20% ili zilipie gharama za mabomba hayo pamoja na vitu vingine kama pampu na compresor kwa ajili ya kusafishia kisima.

Huyo bosi alikubali akasema sawa kesho atakuja na hizo hela. Ilipofika kesho yake mafundi waliendelea na kazi yao ilipofika mida ya saa tano wachimbaji walikuwa tayari wameshalimu mita 100 za kisima ikabidi kiongozi wao ampigiye simu mwenye kisima kuwa anatakiwa alete zile pesa maana wanahitaji kuagizia bomba kutoka mjini ili ziweze kuja, boss akasema sawa nakuja.. baada ya kusema hivyo huyu kiongozi wa wachimbaji akaamua kuondoka kuelekea mjini ili kufuatilia masuala ya mabomba hayo alipokuwa njiani akapigiwa simu na mwenzie aliyemuacha saiti kuwa mwenye kisima kaja lakini kagoma kutowa hiyo hela kasema kuwa 80% aliyokupa inatosha kabisa kumaliza hicho kisima kwa hiyo 20% yako atakulipa ukishayaona maji. huyo kiongozi wa wachimbaji akaamuwa kumpigia simu huyo boss mwenye kisima na akamwambia kuwa mbona unakwenda kinyume na makubaliano yetu, wakati tulikubaliana 20% itoke pale tutakapotaka kuweka bomba lakini ww hutaki?

Hivi unajuwa madhara ya kisima chenye maji mengi kilichokwisha limiwa halafu kikalala bila kuwekwa bomba kuwa kuna uwezekano mkubwa hicho kisima kikakatika chote au sehemu ya kisima hicho? lakin bado akawa mbishi ikabidi huyu fundi awasitishe wale watu waliokuwa wanapeleka bomba saiti maana hakuna hela ya kulipia huo mzigo.


Ikabidi jamaa akope sehemu hela kesho yake akaenda tena saiti na kukuta kisima kimekatika mita 30 za chini, na kisima kikishakatika huwezi kukiendeleza ikabidi jamaa aagize bomba za mita 120 zilizo baki na akazilipia kwa hela yake ya mfukoni hiyo aliyokopa sass ilipofikia hatua ya kuweka kuvuta maji ikaonekana kuwa kisima hakijafika mita zinazotakiwa na pia maji ni machache sana ikabidi mwenye kisima amwambie huyu fundi kuwa achimbe kisima kingine kwa gharama zake au amlipe gharama zake alizotumia kuchimbia kisima ambazo ni millioni 10 jamaa hizo hela hana ikabidi mwenye kisima aende polisi na polisi wakafungua kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kwa sasa kesi ipo mahakamani na jana mashahidi wametoka kutowa ushahidi wao. Je kwa kesi kama hii unamshauri nini huyo fundi wa kisima na jee kama akikutwa na hatia anaweza kupewa hukumu gani.

Nb: hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa jamaa amelipwa millioni 10 ila kuna risiti inayoonesha kuwa jamaa amelipwa millioni 8.

karibuni kwa michango yenu ya kisheria
 
hakuna hata anayefahamu humu kweli?
 
Kiukweli kama makubaliano ya kazi unalipa advance kazi ikishamalizika kabisaaaaaa,,ndio unamalizia hela iliobaki
Hata mimi siwezi kukubali kuwa sijayaona maji yakitoka kwenye bomba ya kisima yaani kiwe kimeshajengewa na bomba nitoe hela
Kwamaana mafundi ukishawapa pesa yote hali ya kuwa kazi haijaisha hio itakula kwako.

Kwa mfano mimi alinitoa jasho mpiga rangi tu[emoji3]
Tulikubaliana kupaka rangi vyumba vi3 laki na nusu nikampa elf80 kama advance,na vifaa vyote nikamnunulia
Baada ya siku 2 akiwa amemaliza kupakaa vyumba viwili akanifata na kunambia kuwa mwanae kalazwa nimpe elf70 kwa huruma yangu nikampa jumla ikawa laki na nusu
Kitokeo cha hapo hadi leo hajaonekana na hata simu yangu hapokei[emoji3]
Kazi hakumaliza na pesa kavuta zote[emoji3]
 
kisheria fundi anashinda hiyo kesi...lbd hakimu apewe rushwa!
 
sasa hapo itategemea na mkataba wenu
 
sasa hapo itategemea na mkataba wenu

Hakuna mkataba zaidi ya kulipa advance kabla ya kazi kisha maliza kazi nikumalizie haki yako iliobaki
Hii inafahamika ulimwenguni

Wewe ukimlipa mtu bado hajamaliza kazi yako utakuwa punguani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…