Naomba ushauri wa kisheria katika maisha haya ya ndoa

Naomba ushauri wa kisheria katika maisha haya ya ndoa

kanyembwe

Member
Joined
Apr 17, 2017
Posts
94
Reaction score
223
Mimi ni Mwanaume mwenye umri wa miaka 45, ni Mkristo dhehebu KKKT, mwaka 2001 nilifunga ndoa ya Kikristo na nimefanikiwa kuwa na watoto 5, mwaka 2007 kulikuwa na mgogoro mkubwa katika ndoa uliopelekea kutengana kwa muda wa mwaka mmoja

Wakati huo tulikuwa na watoto 2, wakati tumetengana nilikutana na mwanamke mwingine na nilimpa mimba, lakini alienda chuo akiwa na mimba mbali na mimi, niliendelea kumpa matunzo akiwa chuoni lakini mke wangu naye alijirudi na tukaendelea na maisha

Hivyo nikawa naishi na wake wawili lakini bi mkubwa hakuju, niliendelea na maisha hayo lakini katika wakati mgumu, bahati nzuri nilienda chuo kusoma na huko nako nikazaa na mwananke mwingine, kwa ufupi hao wote naishi nao na wanafahamiana

Bi mkubwa sasa ana watoto 5 wawili wa kike na wakiume 3, mke wa pili ana watoto wawili wote wa kiume, bi mdogo ana watoto 3 wawili wa kiume na wakike mmoja, nimetoa mahari kwa mke wa pili na bi mdogo, wote ni wakristo, bi mkubwa nimeishi naye miaka 18 sasa

Mke wapili nina miaka 11 na bi mdogo miaka 7, kila mmoja ana kwake na nina mashamba kadhaa na viwanja mbalimbali, je sheria inasemaje kuhusu khaki ya kurithi mali, nikiwa hai au nikiwa nimekufa kwa bahati mbaya, naomba sana mnishauri kisheria zaidi

ahsanteni
 
Mimi sijasoma sheria lkn tafuta mwanasheria andika "will and testament" mapema, weka mgawanyo wowote wa mali zako unaoutaka. Hamna will inayoweza kupingwa popote ukiwa haupo.


Kwenye uandishi; uandishi wako unachosha kusoma! Huwezi kuandika sentensi moja yenye maneno zaidi ya 300 kwa kutenga na koma tu. Hamna uandishi wa hivyo, unakera na unachosha kusoma.
 
Acha ujinga mkuu hakuna mkristo anae owa wanawake wawili mke halali ni mmoja tuu hao wengine ni masuria tu, pia uwe unasoma ulicho andika kabla ya kuposti
 
Mkuu kwa nini uzinzi mwingi hivi?
Mkuu hayo nilishayafanya, sina jinsi nawapenda wanangu na hata wake zangu, nahitaji tu ushauri wa kisheria ili wote wapate khaki sawa, yashatokea ninachohitaji ni kusonga mbele
 
Mimi sijasoma sheria lkn tafuta mwanasheria andika "will and testament" mapema, weka mgawanyo wowote wa mali zako unaoutaka. Hamna will inayoweza kupingwa popote ukiwa haupo.


Kwenye uandishi; uandishi wako unachosha kusoma! Huwezi kuandika sentensi moja yenye maneno zaidi ya 300 kwa kutenga na koma tu. Hamna uandishi wa hivyo, unakera na unachosha kusoma.
Kasoma chuo eti duu bora mimi nilie ishia chekeche A K A vidudu
 
Ushauriwe nini mkuu? Mali si za watoto..

Cha muhimu apo mtafute Demiss akuzalie na yeye apate mali kidogo... maana sijui uo ukristu ni wa nchi gani


Huu ni "Ukristu" wa "Israel", ila bora yeye amesema uweli wake, kuna wengi tu wako hivyo na wanafanya "mambo" yao kimyakimya - Kama "Gwa....Boy".
 
Mimi ni Mwanaume mwenye umri wa miaka 45, ni mkristo zehebu KKKT, mwaka 2001 nilifunga ndoa ya kikristo na nimefanikiwa kuwa na watoto 5, mwaka 2007 kulikuwa na mgogoro mkubwa ktk ndoa uliopelekea kutengana kwa muda wa mwaka mmoja, wakati huo tulikuwa na watoto 2, wakati tumetengana nilikutana na mwanamke mwingine na nilimpa mimba, lakini alienda chuo akiwa na mimba mbali na mimi, niliendelea kumpa matunzo akiwa chuoni lakini mke wangu naye alijirudi na tukaendelea na maisha, hivyo nikawa naishi na wake wawili lakini bi mkubwa hakuju, niliebdekea na maisha hayo lakini katika wakati mgumu, bahati nzuri nilienda chuo kusoma ba huko nako nikazaa na mwananje mwingine, kwa ufupi hao wote naishi nao na wanafahamiana, bi mkubwa sasa ana watoto 5 wawili wa kike na wakiume 3, mke wa pili ana watoto wawili wote wa kiume, bi mdogo ana watoto 3 wawili wa kiume na wakike mmoja, nimetoa mahari kwa mke wa pili na bi mdogo, wote ni wakristo, bi mkubwa nimeishi naye miaka 18 sasa, mke wapili nina miaka 11 na bi mdogo miaka 7, kila mmoja ana kwake na nina mashamba kadhaa na viwanja mbalimbali, je sheria inasemaje kuhusu khaki ya kurithi mali, nikiwa hai au nikiwa nimekufa kwa bahati mbaya, naomba sana mnishauri kisheria zaidi ahsanteni
Kweli mkuu umetekeleza agizo la Mheshimiwa hata kabla hajaingia madarakani
 
Sasa mbona pale juu ulisema umefanikiwa kuwa na watoto 5 wakati unao 10; au ulimaanisha watano wa kwenye ndoa tu?

Btw tafuta Mwanasheria akuongoze uandike wosia mapema; kila mtu apewe mgao wake . Haya mambo ya kuwa na familia kumi kumi; ukitangulia kufariki huku nyuma hapakaliki.
 
Una watoto 10, mwaka 2019 bado kuna watu wanazaa watoto10???
 
Acha ujinga mkuu hakuna mkristo anae owa wanawake wawili mke halali ni mmoja tuu hao wengine ni masuria tu, pia uwe unasoma ulicho andika kabla ya kuposti
Unajua ndugu yangu, haya mambo yamewatokea wengu, hivi ni bora kuwa na wake wawili au wanne wanaojulikana na kujiheshimu, kuliko kuwa na mke mmoja wa ndoa na vimada 5 au zaidi, hili jambo linawatokea wakristo wengi, ndio maana ukimwi uko kwa wanandoa zaidi hasa wakristo kuliko waislamu, ni kwa sababu ya kuwa wanafki katika ndoa, huo ndio ukweli
 
Nilichoona:
Huyu mleta mada huenda sio Mkristu,anataka kuuchafua ukristu unaozingatia ndoa moja tu hadi kifo.
Amekuja kujionesha kuwa naye ana nyumba nyingi za kuwapa wake 3 na kubaki,amekuja kujionesha kuwa naye ana weza kwichikwichi kwa ufasaha.
Kama wewe ni graduate kwanini usiende kwa wanasheria wakushauri hadi uje humu JF ambako wengi ni bush lawyers?
Acha hizo aisee!!
 
Mimi ni Mwanaume mwenye umri wa miaka 45, ni mkristo zehebu KKKT, mwaka 2001 nilifunga ndoa ya kikristo na nimefanikiwa kuwa na watoto 5, mwaka 2007 kulikuwa na mgogoro mkubwa ktk ndoa uliopelekea kutengana kwa muda wa mwaka mmoja, wakati huo tulikuwa na watoto 2, wakati tumetengana nilikutana na mwanamke mwingine na nilimpa mimba, lakini alienda chuo akiwa na mimba mbali na mimi, niliendelea kumpa matunzo akiwa chuoni lakini mke wangu naye alijirudi na tukaendelea na maisha, hivyo nikawa naishi na wake wawili lakini bi mkubwa hakuju, niliebdekea na maisha hayo lakini katika wakati mgumu, bahati nzuri nilienda chuo kusoma ba huko nako nikazaa na mwananje mwingine, kwa ufupi hao wote naishi nao na wanafahamiana, bi mkubwa sasa ana watoto 5 wawili wa kike na wakiume 3, mke wa pili ana watoto wawili wote wa kiume, bi mdogo ana watoto 3 wwa hai hakuna wa kukuingilia kwenye mali zako hata mke mmoja akitangulua. Mke mkubwa ana haki ya kumiliki mali nyingi hao wengine watafutie zao kabisaaa . Usiulize tena kwa awili wa kiume na wakike mmoja, nimetoa mahari kwa mke wa pili na bi mdogo, wote ni wakristo, bi mkubwa nimeishi naye miaka 18 sasa, mke wapili nina miaka 11 na bi mdogo miaka 7, kila mmoja ana kwake na nina mashamba kadhaa na viwanja mbalimbali, je sheria inasemaje kuhusu khaki ya kurithi mali, nikiwa hai au nikiwa nimekufa kwa bahati mbaya, naomba sana mnishauri kisheria zaidi ahsanteni
Mkuu zingatia huu ushauri. Vinginevyo utaleta matatizo. Umesema kila mtu ana kwake. Amua sasa kila mmoja amiliki vyake kwa sasa ukiwa hai. Kama nyuma kila mmoja andikisha yake. Kama mashamba kila mmoja mpe au mtafutie lake na watoto wake. Kusiwe na mgao wa mali baada ya wewe kufa ila si lazima wewe uanze kufa.
 
JAMANI TATIZO LAKE LIKO PIA KWA WENGI WETU CHAMSINGI APEWE USHAURI KWANI NDICHO ALICHOOMBA, matusi na masimango hayasaidii’ yawezekana wewe unaekejeli na kutukana nawe umezalisha mke na umemtelekeza kabisa bila hata matunzo au unaishi na mke hata ndoa hamjafunga, acha ushabiki mandazi!
 
JAMANI TATIZO LAKE LIKO PIA KWA WENGI WETU CHAMSINGI APEWE USHAURI KWANI NDICHO ALICHOOMBA, matusi na masimango hayasaidii’ yawezekana wewe unaekejeli na kutukana nawe umezalisha mke na umemtelekeza kabisa bila hata matunzo au unaishi na mke hata ndoa hamjafunga, acha ushabiki mandazi!
Ahsante sana kwa kujali pia nashujuru kwa ushauri hapo juu,
 
Mimi ni mkristo lakini nikiisoma Biblia hua naielewa vizuri kwamba mwanaume kua na wake wengi siyo dhambi, au kuna mtu anaekijua kifungu cha kwenye Biblia kilichoandikwa kuoa wake zaidi ya mmoja ni dhambi akilete hapa watu tujifunze.
 
Kwanza nakupongeza sana kwa kula mema ya dunia ungefuata misingi ya dini ungekosa kula asali za dunia cha msingi kula mke arithi na watoto wake cha msingi endelea kula bata
 
Sasa mbona pale juu ulisema umefanikiwa kuwa na watoto 5 wakati unao 10; au ulimaanisha watano wa kwenye ndoa tu?

Btw tafuta Mwanasheria akuongoze uandike wosia mapema; kila mtu apewe mgao wake . Haya mambo ya kuwa na familia kumi kumi; ukitangulia kufariki huku nyuma hapakaliki.
maiti wataiacha mortuary wanatwangana kugombea mali atazikwa na city huyo shauri yake
 
Hiz propagana uchwara, watoto 11, unawalisha majani labda,
 
Back
Top Bottom