Naomba ushauri wa kisheria kuhusu Vodacom Mpesa

Daaah!! Mimi nalia na watu wa tigo tangu juzi. Nilituma 66,500 kwenda katika number ya Voda ujumbe ukaja pesa imeenda ila cha ajabu hadi leo haijafika kwa muhusika. Jibu lao ni TUNASHUGHULIKIA
 
Daaah!! Mimi nalia na watu wa tigo tangu juzi. Nilituma 66,500 kwenda katika number ya Voda ujumbe ukaja pesa imeenda ila cha ajabu hadi leo haijafika kwa muhusika. Jibu lao ni TUNASHUGHULIKIA
Bora wewe una siku mbili tu.
 
Usiwasingizie vodacom, tatizo lipo kwenye system za benki, wameanzisha huduma hizi wakati wanajijua hawana uwezo. Mimi nami yamenikuta zaidi ya mara tatu kwa CRDB na sim banking yao hadi sasa nimeacha kutuma pesa kwenda bank kwa kutumia mitandao ya simu. Ukipiga voda wanakwambia pesa zipo bank, ukiangalia account hakuna. Nilivyofuatilia bank wakaniambia niandike barua na kuambatanisha na risiti ya muamala, ndipo wakaingiza, nikawalaumu nini maana ya kuleta huduma ya simbanking, maana yake tunaepuka foleni za benki.
 
Malalamiko yote juu ya uendeshaji wa mitandao ya simu huanzia TCRA. Jaza complain forms zilizo katika website ya TCRA hapo utasaidiwa

Pia jedwali hilo litakusaidia.
Nimetumia hizo email kuwajulisha
 
Sasa ndugu tusiwalaumu kwa nini? Wewe kama unakaa mjini wezako tuko shamba, nimepiga simu hapo siku za mwanzo nikapewa siku 10 za kazi zimepita, baadae zikafika siku 20 na sasa mwezi mzima wamebadiri na kuanza kuniambia niwapigie Shivacom!!! Na namba za Shivacom wamenipa sasa mimi nilituma pesa kupitia Vodacom Mpesa ama Shivacom?
 
Ulituma kwenda bank gani? Pesa yako haipotei kwenye mitandao ya simu
 
Mi nilituma toka nmb kwenda voda. Voda hazikufika na nmb zimesepa nikaenda kote kila mtu anarusha mpira nikaona time is more than my amount of money. Kuanzia hiyo siku nimeacha rasmi kutuma pesa toka bank kwenda kwenye simu au kwenye simu kwenda bank. Bado hawajajipanga na huduma si salama maana ukireport issue inakuwa kama ugomvi majibu ni ya karaha. Hela inatoweka kirahisi unatumia gharama kubwa kufuatilia kuliko thamani ya pesa.
 
Nimekutana na watu wengi sana wenye tatizo kama hili chamuhimu ni kujipanga na kuwapeleka mahakamani tu maana ni pesa nyingi mno waliyohodhi bila utaratibu na wao wanaendelea kuifanyia biashara, mfano nilikutana na mzee naye alikua akifanya malipo ya deni lake Access bank cha ajabu hiyo pesa mpaka leo hajafika ni mwezi wa tatu huu
 
Hata mimi nahisi wanazifanyia biashara mchana kweupe
 
Pole wewe mwenzangu Mimi toka tarehe 10/5/2016 nadai mpesa pesa walizochukua kwenye mpesa na kuninulisha vifurishi internet vya elfu 10 mpaka pesa aikaisha ndio ikawacha elfu 40 nilipodai wakaniomba samahani kwa ni tatizo limetokea wakati wanabadilisha kutoka G 1 kwenda G 2 hivyo watanirudishia hela zangu baada ya SAA 72 saa 72 mpaka Leo hii tarehe 7/9/2016 sijapewa hela nimepiga simu Mara zaidi ya 20 ataa Sijui nifanyaje !!??
 
Ngoja niwaitie hapa waje kusikiliza malalamiko yenu..wapo humu cc Vodacom Tanzania
Power to you
 
Ushauri. Ukituma pesa kwa kutumia mobile banking na haijafika upande ule uliotumia kutuma. Kama umetuma bank m pesa komaa na bank na kama ni m pesa kwenda bank haijafika we komaa na m pesa. Vinginevyo hutopata majibu ya kueleweka utaona wanakuchanganya tu
 
Tayari wameshanichanganya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…