Jamani nina uchungu mkubwa sana. Mimi mungu hakunipa watoto kwahiyo mambo yangu mengi wananifanyia watoto wa wadogo zangu. Mnamo february nilimruhusu mtoto wa mdogo wangu aue sports ream 4 ambazo niliuziwa na mtu aliyeniuzia gari langu rav4. Wakati namruhusu kwamaba alete wateja waone pale pale nyumbani kwangu ndio nikabahatika kumuona anawaonyesha reams hizo nne, nikamwambia mwanangu naomba kila anayetaka kuangalia aje hapa hapa lakini usimruhusu mtu kuzichukuwa na kuzipeleka mahali.
Kiajana wangu akiwa na mmoja wa hao wapangaji wangu, akatetea hoja na kuseama, "hapana mama waache wachukuwe ili watu wazione". Nikamwambia hivi unajuwa mtu akichukuwa mali yako ataiuza kwa bei ambayo hutaifahamu? Na lini ameuza hutafahamu pia?
Kwa ufupi reams ziliuzwa na siku moja wakampigia simu dogo tumeuza matairi lakini yalikuwa mabovu kwa hiyo hela wewe chukuwa laki moja. Kijana wangu hakuniambia na akajadiliana na mama yake mzazi na bila hata kuniambia mimi akawa amerudisha hiyo hela kwao wauzaji.
Siku moja baada ya kukaa sana nikakumbuka nikamuuliza , hivi mwanangu mpaka leo reams zipo wapi?
Kwa ufupi ndio akaniambia wanasema matairi yalikuwa mabovu kwahiyo wanasema hawajapata kitu. Nikamwambia mwanangu, hivi matairi yangekuwa mazima ningeyaacha hapa nisiyatumie? Mbona mimi nilikuwa nauza sports ream?
Kwa ufupi nikawapigia simu na kuwatishia kwenda polisi. Wakamwita kijana wangu nikiwa mimi niko kazini na kumwambia wanakwenda kuchukuwa laki mbili mjini na kisha watampa na kisha zingine watamalizia mwezi march . Nikamwambia hapo hapo watakapo kupa hizo hela muandikishiane. Wakaja mchana wakampa hizo laki 2, kisha wakaandikishiana kwamba zimebaki laki mbili na wakaweka saini zao na jina la atakayelipa.
Kwa ufupi hakuna kilicholipwa na huyu dogo akawa amesafiri akenda morogoro mwezi huo huo walioahidi kulipa akarudi may. Mimi nikamwambia uende mwenyewe serikali ya mtaa ukadai hela yangu maana wewe ndiye uliyeandikishiana nao na hujanitaja mimi kwamba ndiye mwenye mali
akaenda tarehe ya kikao ikapangwa na huyu dogo akitokea kinyerezi kuja mtaa wa bora temeke kwenye case akachelewa, baada ya kufika katibu wa kikao hakutaka hata kumsikiliza.
nikaamua kwenda kufungua hii case mwenyewe na nikaenda na mdogo wangu ambaye walimpigia simu april kwamba aje achukuwe hela ya mama ambapo hakuna walichompatia.
Nilipofika mwenyekiti akaniambia mdeni wako alikuja asubuhi na akasema hana hela
nikamwambia naomba nimpigie aje na hao wenzake ili niwasikilize.
Mdogo wangu akawapigia simu wakaja zaidi ya saa moja limepita.
Kikao kikaaza na wakasema wao hawana hele ya kulipa na mdogo wangu akawaambia kwa nini mimi mlinipigia simu kwamba nije kuchukuwa hela ?
Na kwa nini mliandikishia hii karatasi na dogo, kwamba zimebakia laki mbili ambazo mtalipa march?
Mdogo wangu akaitoa ile karatasi mbele ya kikao.
Wakajibu ,"hiyo ilikuwa tu ni kama danganya toto kwamba tumelipa laki mbili na hatuna zingine kwanza aliyenunua anasema atayarudisha matairi hayo mwezi august maana ni mabovu.
Nikawajibu kwa hasira hivi ninyi mna akili kweli? Mali iliyonunuliwa ikaenda huko inaweza kurudishwa tangu february mpaka august irudishwa? Wakati mnauza hiyo mali mlinipigia simu mimi au huyo dogo na kuniambia mmepata mteja na anasema atatoa bei gani?
Wakajibu sisi hatukupatana lolote na mwanao kwahiyo tuliuza kwa bei tuliyopatana na mteja na tulichopata ndio hicho hatuna kingine labda tukulipe elfu 20 ,20 kila mwezi mpaka deni liishe
kwa ufupi nilitoka nje nikawaacha mwenyekiti na mdogo wangu nikaona hapa ninaweza kumpiga mtu nikapoteza heshima yangu.
Naomba nisaidieni case kama hii kisheria ikoje? Maana karatasi iliyoandikwa na mwenyekiti serikali za mitaa inasema watalipa hilo deni kabla ya mkataba wao kwisha mnamo september 01
kweli hapa haki imetendeka?,
wapendwa ninaomba ushauri wenu, je naweza kwenda mbele kama polisi?