Naomba ushauri wa kisheria

Naomba ushauri wa kisheria

tafakari kali

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2012
Posts
211
Reaction score
39
Habari wanasheri wa jamvi hili.
Naomba ushauri wa kisheria juu ya tatizo langu,ni hivi,mimi nina gari yangu ndogo ambayo nilimpa kijana kwa ajiri ya kufanyia biashara maeneo ya kimara kwa lengo la kujipatia kipato niweze kuendesha maisha, siku moja kijana niliyempa gari alifatwa na jamaa mmoja hivi na kumuomba amwazime gari ana wagonjwa anawapeleka hospital sinza,kwakuwa anamjua na anajua kuwa baba yake huyo jamaa ni mgonjwa anasumbuliwa na mguu kwa miaka mitatu mfululizo alimpa gari na elfu 10 ya kuongeza mafuta. Yule jamaa alipoondoka na gari kumbe akwenda hospital kama alivyosema wakati anaomba gari,yeye alikwenda kufanya tukio la kiarifu la uporaji wa pikipiki,kwa bahati nzuri hawakufanikiwa na watu walitoa msaada kwa mtu wa pikipiki na kuondoka zake,yeye na wenzake walikimbizwa na raia wema,yeye akanusurika kwa kukimbilia kwenye nyumba ya jirani ambaye alimpa hifadhi ma kuwaita polisi,polisi walifika baada ya muda mfupi na kimchukua mtuhumiwa wa wizi na gari(bahati yangu ni kuwa raia wema hawakujua kama wapo na gari langu pengine lingekuwa majivu sasa). Yule dereva wangu baada ya kuona muda mwingi umepita alipatwa na wasiwasi na kuanza kumpigia simu huyo aliyemwazima,anasema mwanzo alikuwa anapokea simu na kumwambia yupo sinza lakini kila alipikuwa akimuuliza mbona hurudi alikuwa anazungusha maneno mara aseme amepata pacha na sababu nyingine zisizo na ukweli,asubuhi mida ya saa 12 ndo ulikuwa mwisho wa mawasiliano yao na wakati huo alikuwa naye anaelekea sinza hospital anasema alishaingiwa na wasiwasi alidhani gari imeibiwa,alifika sinza hospital lakin hakukuta kitu. Akaenda kutoa ripoti kituo cha mabatini ambacho walimwambia arudi kimara ambapo alitoa taarifa na ndipo mie nilipojulishwa. Haya ndo maelezo ya tukio.
Sasa kisheria nawezaje kupata gari langu katika tukio la namna hii? Nimejaribu kufatalilia polisi bila mafanikio.
Nawaomba sana msaada wenu,Natanguliza shukrani zangu.ASANTENI.
(maelezo ya kuwa jamaa alitaka kufanya uharifu na namna ilivyokuwa niliambiwa nilipofika kituoni)
 
Maelezo yako yamenyooka as if ulikuwa eneo la tukio,anyway naweza kkuwa si mtaalamu sana wa masuala ya kisheria ila kwa mazingira ya kawaida gari lako ni kielelezo kimojawapo katika ushahidi wa kesi na kwa vyovyote itachukua muda kabla ya mamlaka husika kuliachia! Ila kikubwa inatakiwa iwe funzo kwa wengine!
 
Sikuwa eneo la tukio ila nilipofika polisi kimara kijana wangu akanieleza hayo maneno ambayo nimeyaeleza hapo.na Kuhusu kujua amefanya uharifu niliambiwa nilipofika kituo cha polisi, Asante sana kwa ushahuri pia.
 
Siyo katika suala hilo tu ila kwa uelewa wangu mdogo huwa najua kwamba kielelezo chochote kinachohusiana na kesi/shauri lililo mahakamani/polisi kitaendelea kushikiliwa tu hadi kesi itakapomalizika ikiwa kuna kesi!
 
Back
Top Bottom