Naomba ushauri wa Mbegu ya nyanya ya muda mrefu

Naomba ushauri wa Mbegu ya nyanya ya muda mrefu

Mayu

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2010
Posts
7,621
Reaction score
12,505
Wadau mimi nalima sana mazao kama vitunguu, hoho, biringanya, bamia. Nimetenga nusu heka nataka nilime nyanya yenye kusapotiwa na miti ambayo inasemekana mavuno ni zaidi ya miezi 3.

Naombeni kama kuna mdau anajua jina la hii mbegu na utunzaji wake.

Nataka nifanye majaribio kwanza, nipande mwezi ujao ili mavuno nianze mwezi wa 12 ambapo nyanya inakuwa adimu kweli kweli kwa huku Singida.

Naombeni ushauri.
 
Milele f1
Harvest 180000 tonnes per acre
Long harvest up to 6months
 
Mkuu bei imesimama ngapi kwa ujazo/uzito mdogo
Nataka nilime nusu eka tu
Asante
Wamepaki kwa idadi ya punje za mbegu paketi ndogo ni mbegu 500 kwa mwakka jana pale Morogoro ilikuwa shilingi elfu 35.
 
Mimi nimesia miche ya jarrah F1 Kampuni ya Rijk zwaan of course sio mingi ni kwa nyumbani tu kama miche 200 na nimechanganya na Victory F1, Mbegu za F1 zinafanya vizuri karibu zote kwa maana ya mavuno asila F1 ni ya muda mrefu. inachumwa mpaka miezi sita kama sikosei.

Tafadhali zingatia haya unapolima nyanya
1. udongo usiotuamisha.
2. Kusiwe na mvua nyingi kama ni outdoor farming. yaan siyo green house.
3. Lazima upandie na mbolea
4. Piga dawa ya wadudu na ukungu kama rido mil gold, multipower n.k ukishapeleka miche shamba isizidi siku 14 tangu kupiga dawa.
5. Weka mbole ya kukuzia kama nitrabo baada 14 days, na zikikaribia maua weka mbole ya yaramila winner au hata urea ya kawaida.
6. fanya huduma nyingine kama kupunguza matawi na kutoa magugu.
kumbuka nyanya inavokuwa matunzo yanazidi.
 
mimi nimesia miche ya jarrah F1 Kampuni ya Rijk zwaan of course sio mingi ni kwa nyumbani tu kama miche 200 na nimechanganya na Victory F1, Mbegu za F1 zinafanya vizuri karibu zote kwa maana ya mavuno asila F1 ni ya muda mrefu. inachumwa mpaka miezi sita kama sikosei.

tafadhali zingatia haya unapolima nyanya
1. udongo usiotuamisha.
2. Kusiwe na mvua nyingi kama ni outdoor farming. yaan siyo green house.
3. Lazima upandie na mbolea
4. Piga dawa ya wadudu na ukungu kama rido mil gold, multipower n.k ukishapeleka miche shamba isizidi siku 14 tangu kupiga dawa.
5. Weka mbole ya kukuzia kama nitrabo baada 14 days, na zikikaribia maua weka mbole ya yaramila winner au hata urea ya kawaida.
6. fanya huduma nyingine kama kupunguza matawi na kutoa magugu.
kumbuka nyanya inavokuwa matunzo yanazidi.
Yap hata mm niliwai panda inazaa sana
 
Back
Top Bottom