Naomba ushauri wa ujenz kwenye eneo dogo

Ally780

Member
Joined
Aug 8, 2021
Posts
23
Reaction score
23
Habari zenu wadau?

Natumai hamjambo wakubwa heshima kwenu.

Nina kiwanja changu kidogo ambacho kina 34ft urefu
22ft upana
Ambacho kipo KatiKati baina ya nyumba na nyumba.
Sina mashaka na urefu wa kiwanja kwa sababu mbele Kuna njia na nimeshaacha nafasi ya kutosha lakini napata shida kwenye upana ambao Ni 22ft kabla ya kuacha space Kati ya nyumba na nyumba.

Nilijaribu kuandaa kijiramani kidogo ambacho kina chumba,sebule,jiko na choo ambacho pia hakipo kitaalam.

Ramani hiyo niliiandaa kulinga na ukubwa wa eneo liliopo kwa upeo wa akili yangu.

Naomba ushauri wenu kuanzia kwenye kiwanga mpaka kwenye ramani yenyewe kipi kifanyike ili niweze kufanya marekebisho kulingana na maoni ya wadau.

Naomba kusilisha.
 
Daah. Maadam umeshaweka vipimo kwenye foot, siwezi kukusaidia. Vingekuwa kwenye running meters ingekuwa rahisi kwangu.
 
Daah! Nimecomvert vipimo vyako kwenda kwenye mita, inaonekana kiwanja chako ni kidogo sana. Mita saba kwa kumi!
Ok, squeeze hii ramani ya nyumba ya vyumba viwili iingie hapo.

 
Kijani chumba cha 3X3. Blue chumba cha 3x3. Yellow ni vyoo (yellow + kijani ni choo cha masta) chenye ukubwa wa 2×2.

Hiyo draft ni sebule na nyuma yake kwenye blue ni jiko huku mbele ni verandah.

Imeisha hiyo.

NB: Vipimo vyote ni kwa mita.
 
Kijani chumba cha 3X3. Blue chumba cha 3x3. Yellow ni vyoo (yellow + kijani ni choo cha masta) chenye ukubwa wa 2×2.
Hiyo draft ni sebule na nyuma yake kwenye blue ni jiko huku mbele ni verandah.
Imeisha hiyo.
NB: Vipimo vyote ni kwa mita.
Asante sana kwa ushaur wako mdau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…