Naomba ushauri wa ununuzi wa kiwanja

The only

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2011
Posts
10,805
Reaction score
14,181
Wakuu habarini ndugu.

Ninaomba ushauri ninunue wapi kiwanja kwa sasa eneo linalofikika kirahisi mjini katikati,lenye huduma za umeme,maji,barabara za uhakika mpango wangu kujenga ghorofa moja simple bajet ya kununulia kiwanja ni 25 mil.

Naomba ushauri sio udalali.

Asante.
 
Pongwe, Tanga.
 
Njoo nikuuzie kiwanja kipo kigamboni Kiwanja k imepimwa umeme uko karibu, pamoja na barabara
 
Kama dar nenda kigamboni...

Ingawa ndani ya miaka 5 kutakuwa na tatizo la foleni ya kufa mtu
 
Kama dar nenda makongo juu,au goba kupitia njia ileile ya makongo juu,barabara ni mbovu but wanaitengeneza soon maana budget yake ilishatolewa
 
Ok goba imepitishwa bila kupingwa
 
Mbweni ni kutamu kama mchalo. Baada ya kupanua barabara ya mwenge tegeta hakuna foleni. Lakini bajeti yako ina bidi ufanye mara 2 ya hiyo.
 
Nenda chanika shuka kituo kinaitwa "Italian" mbele kidogo kuna nyumba za nssf kuna viwanja vya serikali vimepimwa hope huwezi jutia hiyo hela yako.
 
daraja si linakamilika?

Mmmmh

Na utitiri wa malori?

Na kama daraja la pale BP ( puma/gerezani) halijapanuliwa hakuna kitachosaidia maana kwa sasa tu wana foleni kutokana na maeneo ya bendera tatu barabara ndogo

Ukija njia ya chang'ombe pale mataa usisema...waulize wa gongo la mboto, tabata na tmk

Kiufupi miundombinu ni hovyo na mji unakua kwa kasi
 
Nenda chanika shuka kituo kinaitwa "Italian" mbele kidogo kuna nyumba za nssf kuna viwanja vya serikali vimepimwa hope huwezi jutia hiyo hela yako.

Uko sahihi mkuu, eneo linaitwa Buyuni ni kuzuri sana. Mm nimejenga kule.
 
Ukishaamua tutafutane ili tufanye mambo, sawasawa?
 
BY:Mkulimasana1
Njoo Iringa nikuuzie kiwanja ujenge hosteli ya wanafunzi karibu na Tumaini University 0768069996/0719786521
 
Kama dar nenda makongo juu,au goba kupitia njia ileile ya makongo juu,barabara ni mbovu but wanaitengeneza soon maana budget yake ilishatolewa
Goba na Makongo naungana nawe na hasa kwa kuwa unaongelea kujenga gorofa.
 
njoo makongo juu kiwanja kipo vizuri sana umeme na barabara ni uhakika..kiwanja kina upana wa meter 22 na urefu meter 17 ...kiwanja kipo karibu na UDSM pamoja na ARDHI UNIVERSITY dar es salaam ...bei million 20 mkuu hakuna udalali wala longolongo
 
daah 22mx17m hilo eneo litafaa kweli kutoa kighorofa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…