Jitahidi ale balanced diet tu, yaani mlo kamili ambao utakua na makundi yote ya vyakula. Ila moja ya vyakula vinavyohitajika kwa wingi ni
1)PROTEIN. apate protein za kutosha ili kusaidia tissue renewal na kuzalisha maziwa ya mtoto wake .(Nyama, maharage, karanga, samaki, maziwa, mayai)
2)IRON + VITAMINS. Vyakula vya madini ya chuma(iron) na vitamins kwa ajili ya kupambana na anaemia maana mama anaweza kua amepoteza damu nyingi kipindi cha kujifungua. (Maini,dagaa,matunda, mboga mboga za majani kama matembele, mchicha n.k )
3) Anywe maji mengi sana na apate mda wa kufanya mazoezi hata ya kutembea + apate muda wa kupumzika (kulala).