tama
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 602
- 71
Nina rafiki yangu ameniomba ushauri afanyeje juu ya hili.Ana mpenzi wake ambaye amemvisha pete ya uchumba ila anasema kuwa msichana amebadilika kupita kiasi na tabia nyingine za ajabu2 ambazo mwanzoni alikuwa hana,amefika mpaka anaanza kumwambia jamaa tukioana ndugu zako wakija kwetu waseme wanakuja lini na kuondoka lini na mama mkwe ndo sitaki kabisa kumsikia akija kwetu kisa mama mkwe alikataa kuhudhuria tukio la binti alipokuwa anavalishwa pete.Na mama alimwambia kijana wake huyu msichana sio mwanagu na mama kuamua kurudi kijijini siku ya tukio hilo ya kuveshwa pete binti,na jamaa ana juta ile mbaya na kusema bora angemsikiliza mama yake.Sasa ameniomba ushauri afanyeje sababu anasema hata akimuoa huyo binti ana amini kuwa ndoa yao haitakuwa na amani na pia anahofia ndugu kumtenga,ameniomba ushauri je amwache binti au afanyeje amechanganyikiwa hajui afanye nini,mawazo yenu tafadhali.