Mapenzi ni kitu cha ajabu sana unaweza kumsaidia huyo mama kila kitu den siku ya kesi akakugeuka na kusema wewe ndo ulimshawishi kufanya hivyo ila bado mume wake anampenda sana utatatamani ardhi ipasuke uingie maana huyo baba kibano kitakugeukia. unaweza kumpa tu ushauri afanye mwenyewe au kumuonyesha njia nina mfano hai ndo maana nimesema hivyo.
Bahati yake wewe siyo mimi maana ingekuwa mimi ningemshughulikia mwenyewe kwa mikono yangu. He is a complete jackass.
Ila unaweza kumdunda mumewe halafu mke akakuchenjia kwa nini umempiga mumewe. Haya mambo bana....sometimes they have no rhyme or reason to them.
Yaani kama usiku wa kuamkia leo mdada kabondwa nilitamani sijui nifanye nini walahi.....................inauma sana kwa kweli.
Asante sana dia.........huyo dada kwa kweli anateseka sana. Ila nilifikiria labda wakati wa pulukushani mi ndio niwaite polisi.
ooh my goodness! pole sana! ni kweli sisi wanawake viumbe vya ajabu sana. kwanza anaweza kusema unamtolea macho huyo upupu wake! empower that woman,ongea nae muambie hastahili kupigwa kwa kosa lolote. tena huyo mumewe atamuua na atapata victim mwingine!jaribu kuongea na familia pia. kama huyo mama hana nguvu ya ku-deal na tatizo lake hata ukienda tamwa bila ushirikiano wake huwezi kumsaidia! duh, i need a heavy lunch just now!
Ongea na huyo mama kwanza, ila pia nakushauri uwe makini unapoongea na mkewe maana wapo majirani wanaweza kupeleka uzushi kwa huyo mwanaume kuwa mna mahusiano ya kimapenzi. Huyo mama mwambie akikubali aende TAMWA watamsaidia, ila kama huyo mama haimsumbui huenda ni sehemu ya mapenzi yao maana kuna makabila mengine kupigwa ni sehemu ya mapenzi
wewe ndio unaeona anateseka but huyo dada yeye haoni kama anateseka ndio mana bado wanaishi pa1, hivi ukawaita hao polisi wakamchukua huyo baba, mkewe akaenda kumtoa utajickiaje? kutafuta matatizo tu!...huyo baba mwenye nyumba akija kujua wewe ndio umewa call hao polic kwa tatizo liclo kuhusu c ndio mwanzo wa purukushani za wenye nyumba?
Asante nyamayao kwa ushauri.
Ila ndugu yangu ukisema halinihusu kidogo napata shida kuelewa. Hivi kwa mfano kama vile alivyompiga usiku wa jana kuamkia leo, yule mdada angekufa au labda kapata kilema cha maisha.........nitajisikiaje? Mi ninavyofahamu yule ni mtu na hastahili kutendewa hivyo anavyotendewa sasa, ndio maana naomba ushauri hapa, nifanye nini ili kumsaidia tu au kumshauri..........lakini pia sitamlazimisha afate ushauri wangu.
unatakiwa ujihurumie kwanza kabla hujahurumiwa, yakitokea hayo yote ni mdada kapenda mwenyewe coz hajihurumii, nakuelewa huruma yako ilipo but mie ninakuwaga sana na hofu ya kuingilia mapenzi ya watu, hayatabiriki...unaweza kuvuna ubaya au uzuri.....kama upo tayari kumsaidia kwa huruma uliyonayo pia uwe tayari kwa lolote kutokea kwa hao wanandoa....goodluck!
Hapo nilibold ndio pananiogopesha sana..........maana jamaa anabonda ile mbaya, kabla ya usiku wa kuamkia jana kuna siku alimdunda mpaka akamng'oa rasta za upande mmoja. Sasa najiuliza siku akimdunda kama mazoea yake na akafa na sisi (wapangaji) tumenyamaza tu, hivi itakuwaje?
Utakuwa umemsaidia sana huyo mama kwa kuongea nae na kumwelewesha haki zake na kwamba hapaswi kupigwa hata kama amekosa kosa kubwa kiasi gani.Na umweleze madhara ya kuendelea kupigwa ni kilema cha maisha au kifo,Pia mwambie avumilie vingine lakini si kipigo cha kumweka mapengo au kumtia ulemavu.
Akishajua haki zake ni rahisi kwenda polisi yeye mwenyewe.
Aisee wewe kimbelembele chako kitakutokea pabaya!!!Mambo ya ngoswe mwachie ngoswe mwenyewe.Kwetu kule Ukuriani mwanamke kupigwa ndo kupendwa kwenyewe.Unajuaje kama ndo mapenzi yao??Kaa mbali,Tafuta kwako nawe yakukute.Huna adabu sana wewe ,Ukimpeleka baba polisi wewe utawapa msosi??Au utamsomeshea wanae wakati anaenda lupango??Una lako jambo mpangaji weee? Kwani umepanga hapo kuwa contable wa mwenye nyumb??? hufai wewe- nenda zako.
Aisee wewe kimbelembele chako kitakutokea pabaya!!!Mambo ya ngoswe mwachie ngoswe mwenyewe.Kwetu kule Ukuriani mwanamke kupigwa ndo kupendwa kwenyewe.Unajuaje kama ndo mapenzi yao??Kaa mbali,Tafuta kwako nawe yakukute.Huna adabu sana wewe ,Ukimpeleka baba polisi wewe utawapa msosi??Au utamsomeshea wanae wakati anaenda lupango??Una lako jambo mpangaji weee? Kwani umepanga hapo kuwa contable wa mwenye nyumb??? hufai wewe- nenda zako.