Naomba ushauri

Joined
Nov 12, 2011
Posts
8
Reaction score
0
Nilikuwa na msichana mmoja niliunganishiwa na dada yake na huyo msichana,sasa siku ya kwanza kukutana siu ileile yule msichana akaniuliza nimevutiwa na yeye ama hapana mimi nikakubari nimevutiwa nae,ni kweli alikua na vitu baadhi navikubali kwake,siku mbili baada ya kuonana nikaandikiwa na yule dem akidai TUACHANE akiwa na visingizio eti yeye akikosa vocha ya kunitumia sms anaumia sana wakati time zingine nilikua nina mtumia vocha,sababu nyingine anadai nimwache na yeye asogee level ya chuo kama mimi wakati huo yupo 4m five mimi nipo diploma,ilo swala tukasuluhisha likaisha mara ya pili tena nikatumiwa sms TUACHANE kwa vigezo vya ajabu ajabu,mara ya tatu tena tukashindana kwa kitu kingine coz yule dem ni mbishi balaa,aliniazimisha kitu chake alipokihitaji akatuma mtu akifate,mimi hapo hapo nikaona huu ni upuuzi japokua dada yake tunaheshimiana sana nikaamua kumpiga chini yule dem,siku ile le akanywa vidonge ajiue bahati nzuri nikampigia sim mfanyakazi wao simu kumjulisha so alipozidiwa akaenda kuwashitua wakubwa wakampatia maziwa akapona,sasa hivi tunawasiliana kimagumashi sana mimi ndo niliamua kupunguza mawasiliano sana,lakini ata hivyo huyu dem hashituki saaana,ila siku akituma sms anaonekana kama mtu ambae bado hajanikatia tamaa,na dada yake bado sijamweleza mpango wa kumwacha mdogo wake,nisaidieni hapo wadau
 
Je ulikuwa na lengo gani hasa wakati unaunganishiwa?
Je ukijitafakari wewe binafsi na huyo binti kuna uwezekano wa kuunda familia?
Je dada yake anao mtizamo gani juu ya mahusiano yenu?
MTIZAMO WANGU: Kati yenu kuna mmoja hajitambui. Siwezi kusema ni binti kwa kuwa sijasikia utetezi wake.
 
Kuwa mwanaume jasiri wewe, kama kitu hukitaki unakipa live kwamba hukitaki kuliko kupotezeana muda, akitaka kujiua na ajiue kwani kila mtu anamaamuzi juu ya maisha yake. Shtuka ndugu yangu, Dunia ya sasa kitu cha kuumiza kichwa ni maisha (pesa) na siyo mapenzi.
 
Mbona unajitesa nafsi yako? kwani hizo vocha ulikua unampa kabla hujaanza kua nae kama mpenzi wako? sababu umesema
Baada ya siku mbili ndio unapewa talaka sasa hayo mapenzi ya siku2 ndio yakupelekeshe puta? ebu jikaze kiume utoe mamuzi...
 
una mda gani na huyo binti ktk mahusiano yenu?ukinisaidia hilo nitajua mahali pa kuanzia kutoa ushauri wng.
 
anayeweza kujiua anaweza kuua pia,,,mpotezee taratibu bado mtoto huyo ananuka maziwa pia hajui nini maana ya kupenda na kupendwa,,,,,tafuta anayejua maana ya kupenda na kupendwa.!!! fanya maamuzi magumu
 
kwanza kiukweli bado sijajua msimamo wa dada yake kuhusu uhusiano wetu lakini dada yake alikua ananisisitiza nimhimize kusoma sana mdogo wake,pili sikua na malengo ya kuunda familia nae bali ni kwa uhsiano wa kimapenzi@Willyguy
 
Hakuna mapenzi hapo ni mdako tu!
 

mapenzi na shule wap na wap dogo,mwache mwenzako asome kwanza....
 
Hawa ndo wametoroka fb wanaandika post Kachumbari yaani ina nyanya,vitunguu,hoho n.k we huoni maneno kama Dem,@ mtiririko wa lugha anyway ndo hivyo tena tutafanyaje tumejitenga ila watoto wanatufuata nyuma kuomba hela za ice cream.
 

umefunga goli Mkuu Mpaka Umeondoka Na Nyavu
Sna Jpya!
 
Nitajirekebisha maneno ya kutumia kaka,naona kutumia neno dem na @ nimekuudhi sio,lakini ushauri wako ninauhitaji mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…