Naomba ushauri

janey1985

New Member
Joined
Mar 12, 2014
Posts
3
Reaction score
0
Hello Dk. Pole na majukumu ya kuelimisha jamii. Mimi ni mama mwenye umri wa miaka 29, nilijifungua mtoto na kuweza kutumia njia ya uzazi ambayo ni njiti ya muda wa miaka mitatu, lakini nilikaa nayo kwa muda wa miaka miwili na kuweza kuitoa, lakini baada ya kuitoa yapata miezi tisa sijaona siku zangu, Naomba unisaidie kutatua tatizo hilo au unishauri nitumie dawa gani ili niweze kupata siku zangu.

ahsante.
 
Mh...ngoja waje, ila kama uliweka ya miaka 3, ukakaa miaka 2 ukaitoa, sasa si bado mwaka mmoja ili kukamilisha mda wa vijiti?

Any way, ukipata ushauri wa hapa jf, nenda na kwa madaktari wanao husika na masuala ya uzazi.
 
pole dada kawaida njia hizi za kisasa zinzvyofanya kazi zina athiri sana mfumo wa asili wa mwili zingine zinaenda kuzuia ovary zisipevushe mayai,zingine zinakwenda kufanya kazi kwenye mfuko wa uzazi yaani kuharibu mazingira ya mimba kupandikizwa,sasa mtu akitumia muda mrefu system ya mwili hushindwa kabisa kufanya kazi yake ndo maana wengine huwa hawawezi tena kupata watoto maana hata hormone zinazopevusha mayai zinakuwa zimeacha kuzalishwa.

Hata hivyo dozi ya hizi dawa inakuwa kwenye mzunguko wa damu kwa muda mrefu kadri siku zinavyozidi kwenda mbele baada ya kuacha kutumia mwishowe huisha nguvu na baadaye mfumo hurejea kama mwanzo inategemea zilikuwa ziumeathiri mfumo wa mwili kiasi gani lakini wengi kuanzia miezi sita na kuendelea mfumo hurudi normal,hivyo endelea kuvuta subira mfumo urudi ktk hali yake.
 
Ahsante kwa maelezo yako, nitavuta subra. Lakini naomba kuuliza juu ya suala la uzazi wa mpango kwa kutumia mbegu za minyonyo, Je ni kweli! na je hutumikaje! Na kama ni NDIYO, kwa mtu mwenye mzungungo mfupi au mrefu zinatumika vipi? Maana nimesikia hii ndiyo njia bora na salama kwa uzazi wa mpango
 
Ahsante kwa maelezo yako, nitavuta subra. Lakini naomba kuuliza juu ya suala la uzazi wa mpango kwa kutumia mbegu za minyonyo, Je ni kweli! na je hutumikaje! Na kama ni NDIYO, kwa mtu mwenye mzungungo mfupi au mrefu zinatumika vipi? Maana nimesikia hii ndiyo njia bora na salama kwa uzazi wa mpango
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…