Taiq
Member
- Feb 14, 2023
- 97
- 86
Ndugu wanajanvi wenzangu mwenzenu nina shida ya kutolipwa sitahiki zangu za likizo kwa kipindi cha miaka sita sasa tangu kupata ajira mwaka 2017. Kwa kipindi chote hicho nimejalibu kufuatilia lakini cjawahi kulipwa. Sasa Ndugu zangu walimu na wanajanvi naomba mnisaidie ni viambatanishi vipi vinahitajika ili mtu aweze kulipwa pesa ya nauli?
Nimeamua kuomba msaada baada ya usumbufu wa muda mrefu kutoka kwa viongozi wangu ambao wamekuwa wakinipiga danadana kama mpira na kutokana na danadana zao wamenidhoofisha kiuchumi mimi binafisi pamoja na familia yangu. Kivipi wamenidhoofisha kiuchumi?
Hii ni kutokana na nauli za nenda rudi ninazotumia zimekuwa nyingi kupita kiasi. Kiukweli mi kama mfanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara idara ya elimu nimeshindwa kufahamu ni wapi nakosea.
Kiukweli nimechoswa na manyanyaso ya watawala maana imefikia hatua sasa mpaka faili kupatikana inakuwa shida.
Ndugu zangu naomba ushauri nifanye nini ili haki yangu niipate.