Naomba utaratibu wa kupata kibali cha kujenga nyumba ya kawaida ambayo sio ghorofa

tidier Ar

Member
Joined
Feb 14, 2020
Posts
32
Reaction score
14
Msaada kwenu ndugu maana saizi sielewi pia uwezo kujenga bila kibali upo lakini shida sitaki kuvunja utaratibu.

MSAADA KWENU
 
Nenda halmashauri ya mji uliopo utapatiwa mwongozo.
 
Msaada kwenu ndugu maana saizi sielewi pia uwezo kujenga bila kibali upo lakini shida sitaki kuvunja utaratibu.

MSAADA KWENU
Unafanya jambo zuri mkuu, Chukua kibali shusha mjengo wako kwa amani.
Ni kwamba taratibu zinategemeana na kama sehemu unayojenga imepimwa au haijapimwa.

Kwa maeneo yaliyopimwa, Utaratibu ni kuandika barua ya maombi kwa mkurugenzi wa halmashauri husika ambayo pia unaambatanisha na nyaraka zako za umiliki wa kiwanja pamoja na michoro/ramani za jengo husika. Sasa kwakua wewe unajenga nyumba ya kawaida utahitaji seti tatu za michoro (architectural drawings) ila kwa wanaojenga maghorofa huwa kuna ongezeko la seti mbili za michoro (structural drawings).

Michoro yote ni lazima iwe na mihuri ya wataalamu walio sanifu. Huwa kuna gharama unalipia ambazo zinategemeana na ukubwa wa jengo kwenye kiwanja, kila halmashauri wana gharama zao.

Ila kama eneo halijapimwa basi utaenda halmashauri idara ya ujenzi watakupa fomu za kujaza, ambazo utatakiwa kwenda kuthibitisha umiliki kwa serikali ya mtaa husika. Kisha utaendelea na utaratibu nilioueleza hapo juu.
Note: kunaweza kuwa na viutaratibu vya nyongeza kwenye baadhi ya halmashauri
 
Kwa maeneo yaliyopimwa, Utaratibu ni kuandika barua ya maombi kwa mkurugenzi wa halmashauri husika ambayo pia unaambatanisha na nyaraka zako za umiliki wa kiwanja pamoja na michoro/ramani za jengo husika.

Sasa kwakua wewe unajenga nyumba ya kawaida utahitaji seti tatu za michoro (architectural drawings) ila kwa wanaojenga maghorofa huwa kuna ongezeko la seti mbili za michoro (structural drawings).

Michoro yote ni lazima iwe na mihuri ya wataalamu walio sanifu. Huwa kuna gharama unalipia ambazo zinategemeana na ukubwa wa jengo kwenye kiwanja, kila halmashauri wana gharama zao.

Ila kama eneo halijapimwa basi utaenda halmashauri idara ya ujenzi watakupa fomu za kujaza, ambazo utatakiwa kwenda kuthibitisha umiliki kwa serikali ya mtaa husika. Kisha utaendelea na utaratibu nilioueleza hapo juu.
Note: kunaweza kuwa na viutaratibu vya nyongeza kwenye baadhi ya halmashauri
 
Ila kama eneo halijapimwa basi utaenda halmashauri idara ya ujenzi watakupa fomu za kujaza, ambazo utatakiwa kwenda kuthibitisha umiliki kwa serikali ya mtaa husika. Kisha utaendelea na utaratibu nilioueleza hapo juu.
Note: kunaweza kuwa na viutaratibu vya nyongeza kwenye baadhi ya halmashauri
Asante ndugu, umenigusa.
 
Unafanya jambo zuri mkuu, Chukua kibali shusha mjengo wako kwa amani.
Ni kwamba taratibu zinategemeana na kama sehemu unayojenga imepimwa au haijapimwa.

Kwa maeneo yaliyopimwa, Utaratibu ni kuandika barua ya maombi kwa mkurugenzi wa halmashauri husika ambayo pia unaambatanisha na nyaraka zako za umiliki wa kiwanja pamoja na michoro/ramani za jengo husika. Sasa kwakua wewe unajenga nyumba ya kawaida utahitaji seti tatu za michoro (architectural drawings) ila kwa wanaojenga maghorofa huwa kuna ongezeko la seti mbili za michoro (structural drawings).

Michoro yote ni lazima iwe na mihuri ya wataalamu walio sanifu. Huwa kuna gharama unalipia ambazo zinategemeana na ukubwa wa jengo kwenye kiwanja, kila halmashauri wana gharama zao.

Ila kama eneo halijapimwa basi utaenda halmashauri idara ya ujenzi watakupa fomu za kujaza, ambazo utatakiwa kwenda kuthibitisha umiliki kwa serikali ya mtaa husika. Kisha utaendelea na utaratibu nilioueleza hapo juu.
Note: kunaweza kuwa na viutaratibu vya nyongeza kwenye baadhi ya halmashauri
Mkuu, mim nina kiwanja changu 17-13 tyr kimepimwa na nimeshazungukwa na makaz je natakiwa kutafuta kibali cha halmashaur kwaajil ya kufanya ujenz? Msaada please
 
Natumae mleta mada umepata muongozo...

Building permit, hua zinacheleweshwa sana...
Unaweza anza kujenga, mpaka unamaliza, unahamia, unaishi miaka kadhaa na kibali bado hakijatoka...

Cc: mahondaw
 
Mkuu, mim nina kiwanja changu 17-13 tyr kimepimwa na nimeshazungukwa na makaz je natakiwa kutafuta kibali cha halmashaur kwaajil ya kufanya ujenz? Msaada please
Ndio boss ni lazima na jamaa kwa baadhi ya halmashauri ni kama wameanza kukaza sana saivi. Wewe nenda halmashauri utapewa walau taratibu za eneo husika kabla haujaanza ujenzi, vingivevyo kuna watu wengi nyumba zao zitageuzwa chakula ya wahusika wa halmashauri.

Unaweza jikuta umejenga ukiwa umekiuka taratibu kibao. Mfano Kinondoni kuna baadhi ya maeneo hawaruhusu kujenga nyumba za chini, Dodoma jiji pia kuna maeneo wanataka ufikishe 'coverage' fulani ndio wakupe kibali ( sio una kiwanja kikubwa halafu jengo halichukui hata 20% ya eneo husika).

Na kwa hicho kiwanja chako (17m x 13m) utaratbu wa kawaida kabisa unatakiwa uache walau mita 1.5 kila upande wa jengo, achilia mbali taratibu nyingine nyingi.
 
Back
Top Bottom