Kwanza pole sana kuchukua muda kufikiri sana. Pili ni jambo la kawaida kujisikia hivyo kwa mtu uliyemfia kimahaba.
Ushauri; tafuta ukaribu na kaka huyo, jitoe hata kumpiga outings kadhaa. Zungumzeni mambo ya maisha mkirejea mlikotoka. Jiheshimu kwake na usijirahisi kiasi hicho. baada ya kuanzisha mawasiliano hayo kwa kipindi fulani utagundua kilicho moyoni mwake. Tunza uadilifu wako -kama unao...huenda na yeye anajisikia unavyojisikia mtakapotumia muda wa kutosha kwenye mahusiano mtafahamiana na kujua kila mtu anayowaza juu ya mwingine.