Naomba wazo la biashara ya usambazaji bidhaa

Bm_boy

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2013
Posts
547
Reaction score
347
Wakuu habari..

Nipo Moshi, nina gari aina ya IST natamani kutumia gari hii inizalishie tofauti nakuitumia kupigia misele mjini.

Naombeni wazo ni bidhaa gani naweza kusambaza kwa wateja kwakutumia hii gari nikapata kipato..
 
Njoo kahama nikuuzie mafuta ya alizet au karanga utakuja kunishukuru
 
Mi pia nipo moshi time hii, nunua bidhaa za dukani( mahitaji ya nyumbani za jumla) uuze maduka ya reja reja.
Nashukuru mkuu nitalifanyia kazi kujua ni bidhaa gani nitaanza nazo, angalau zikanilipa mafuta na hata hela kidogo ya akiba per day..
 
Ngoja waje kukupa muongozo...

Naonaga watu wanaziuzia, matunda, vyandarua, vyombo vya ndani, wanaweka nyuma ya buti wanatega mahali wanaanza wanaacha buti wazi na kuuza...
 
Ngoja waje kukupa muongozo...

Naonaga watu wanaziuzia, matunda, vyandarua, vyombo vya ndani, wanaweka nyuma ya buti wanatega mahali wanaanza wanaacha buti wazi na kuuza...
Asante mkuu.. nitachunguza mkuu kulingana na mazingira..?
 
Nashukuru mkuu nitalifanyia kazi kujua ni bidhaa gani nitaanza nazo, angalau zikanilipa mafuta na hata hela kidogo ya akiba per day..
# Sabuni ya kipande kama jamaa, white wash n.k....unawauzia kwa bei ya jumla wao wauze reja reja.
# Uza Vocha za simu za aina zote jumla...
#Uza pipi, na bublish kwa jumla.
# Uza malapa jumla kwa carton..
# Ukiweza uza juice za energy Kwa carton jumla. Yaani IST ishone πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… angalia usiue shockup mangi....hapo ukikosa faida na pesa ya mafuta kaoge na maji ya mpapai 🀣🀣🀣

Usiuzie mjini moshi sasa utafeli kiasi. Njoo kibosho kwetu, uru, bonite, yaani nje ya mji kidogo, wala usiende mbali sana na mjini mfano usiende sanya au rombo huko mbali sana.

Haloo haya ni madini tupu nakupa mkuu, ingia field, yaani nimekupa elimu ya bureeeee, no charges.
 
Nimekupata mkuu.. nikija kibosho nitakutafta.. kirima au umbwe..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…