Unatokea mkoa gani?
Guest maeneo yale ni mtihani, Ukiingia Dar nenda Kalale Mazese pale guest za kutosha Barabarani kabisa, mfn Silent INN ukimaliza tu kile kito cha mwendokasi kama unatokea ubungo mkono wa kushoto, Chumba kuanzia buku 7 - 12, Asubuhi wahi,
Sio lazima Saa 10, advantage ya kuwahi unachukua mzigo kwa utulivu, vingi vizuri..
Disadvantage ya kuwahi bei inakua juu, kukipambazuka unashangaa tu ghafla wanashusha bei ya mzigo ule ule, wakiami vizuri vyote vishaenda, mda mwingne inaweza isiwe hivyo maana kuna watu wanashika meza kwa masaa, ukifika mda anaachia..
Nikupe mbinu?
Kama unatokea mikoa ya karibu
Mf Pwani, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Moro, lindi, Mtwara, unaweza uka save pesa yako ya guest..
Jioni kaa Main road, SPECIAL HIRE na Privates ni nyingi sana mikoa hio, unaondoka jioni, Kuanzia Saa 9 usiku zinaingia Dar, unashushwa hapo Ubungo.., unazama karume, Saa 3 ushamaliza, kama una zanga nyingine unachukua kariakoo, unawahi mbezi mpk saa 9 gari za hio mikoa ni uhakika, unarudi,
Hujapoteza siku, hujapoteza pesa.
Ukiingia karume acha papala, Sio umeona viatu vinakuvutia, unataka ujaze roba sehemu moja,
Chukua Vichache, zunguka uangalie, unaweza ukapata zaidi ya hivyo kwa bei nzuri pia, la sivyo utafika sehemu utaona mzigo mzuri halafu pesa umemaliza..
EPUKA KUPANIC Ukiona mzigo mzuri, au Mzigo hausomeki.
Kitu cha kwanza ukishika kiatu ni kuangalia Soli na Ungio la soli na kiatu..
Kua makini na wazee wa ndole, kama una begi la pesa weka mbele..
kua makini zaidi na meza utakayoweka/acha/hifadhi mzigo, Kusahau ni rahisi sana, pale pana meza kama 1000, kila ile utaona zinafanana, ukiisahau imekula kwako.
Yapo machimbo 3 hapo karume, ukiwa unatokea K.koo mwisho wa ukuta bila shaka wa serengeti breweries(yaani soko linapoanza) kunja kulia, ukifika mbele utaona barabara ya vumbi kushoto, pita nayo, ukifika mbele kuna Meza za upande wako wa chini, na nyingine upande wa juu, Maeneo yale pana viatu vingi vya kiume, na kwa uzoefu machimbo yale ndio yanakua na viatu vizuri zaidi..
Anza na upande wa chini(meza sio nyingi sana) ukimaliza hamia juu, unapanda taratibu, ukifika juu kabisa meza zinapoishia kama umesharidhika napo, kunja kulia utapita mabanda/fremu kadhaa utakutana na chimbo kubwa sasa, Pale ni full kelele, na ndio hapo ukijichanganya kusahau mziho umeacha wapi basi sahau, kule viatu ni vingi mno, msongamano mkubwa.. Viatu vya kike, watoto na Men zipo za kutosha, Malizia mzigo wako Tafuta guta, toa barabarani Sepa..
Usijichanganye kwa wale wanaotundika viatu unaowaona ukiwa unatoka kuja nje utanyooshwa, wale wamepoint tuu kama wewe wakapiga kiwi, wale wateja wao ni Wanaume wa Dar.
Jumamosi na Jumanne ndio siku nzuri zaidi japo mabadiliko yapo.
Nilikua Ijumaa jioni naingia Dar, jumamosi karume & k.koo, Jumapili asubuhi nipo Shop na pea Zaidi ya 100, kumbuka nikitoka karume naingia kariakoo, kubeba Vifaa vya simu, nguo n.k,
Narudi sina famba, sina reject, mzigo wangu nilikua situmii nguvu, walikua wananisubiri mpk ile usiku nikiingia tuu nawakuta golini wananisubiri, Pointing yangu mpk wale wauzaji walikua wananishangaa, wanasema mzigo ninaochukua kwa masaa 5 watu wengine wanapita nao Siku 4.
Uzuri wa biashara ya bidhaa za kuvaa kama hizi, Usiogope ushindani hata wakuzunguke 100, Ukiwa na jicho la ku point tuu, umemaliza..
Hii sio sukari, eti wote mnauza aliekaribu ndio anapata wateja wengi...
Hapa ni aliye na bidha bora na nzuri hata yupo mwisho..
Ukirudi Shop Kua na bai FIXED na rafiki,
Anaglia mzigo wako ukienda juu sana unanunua kwa sh ngapi, ukiopoa sana unanunua kwa sh ngapi(hapa nazungumzia viatu vya ubora unaofanana lakini kuna siku vinatofautiana bei), soma uchumi wa wateja wako, then weka bei elekezi, epuka kubadilika badilika, kuna picha wateja wataijenga either una tamaa(pale unapopandisha bei) au kuna mda unauzia njaa(pale unaposhusha mzigo), fanya wateja wako wajue bei zako, akija anajia kabisa najiaandaa kwa bei hii, na huko wataambiana, wewe leo umemuuzia huyu kitonga, ngafla jamaa anaenda kuwaambia wenzake "jamaa ameshusha bei" keshokutwa wamekuja unawaambia brah brah eti mzigo godown umepanda.....
Mimi kitu ambacho nilikua nafanya, wengi walikua wanashangaa lakini ndio ikanirahisishia,
Viatu vyoteeeeeeee vya kiume bei ilikua ni mojaa, yaani sikua na ile chagua nikupe bei, hivyo hivyo vya kike na watoto..
Mpk mtu anakuuliza mbona hiki kikali zaidi ya hiki? Unamwambia tuu hivyo viatu vyote ni vizuri, kuna mwenzako atachukua hicho kingine(kwa lugha nzuri lakini).
Sijui una experience ya hii kitu...
Mteja akichukulia kitu poa halafu ukamtajia bei sawa na kile anachokiona kizuri(kwa mtazamo wake)atajiuliza na atakua makini nacho, kuhisi labda ni jicho lake...
Na mimi sababu najiamini na bidhaa zangu, Sishushi, wateja wanatofautiana macho, kila kiatu kilikua kinaenda kwa Wakati wake... ,
Bei fixed inakusaidia pia hata ukiweka mfanyakazi, kutosumbuana na simu za kuelekezana kiatu kilivyo ili ujue bei yake..
Itakusaidia pia kupiga hesabu za mauzo vizuri, unajua kabisa nimeuza pea kadhaa, natakiwa niwe na sh ngapi..
Mwisho hata wateja wataheshimu duka lako, sio mteja anakuja anataja bei ambayo unaona kabisa hizi ni dharau...,
Discounts mara moja moja hasa kwa wateja wanaochukua zaidi ya pea moja, sio mbaya...
Ongea na mteja kwa lunga nzuri, mshawishi kwa ubora
Usimlambe sana miguu, hataki basi sio fungu lako....
Yote haya kama huamini mzigo wako ni BURE,
Kam mzigo ni mzuri hutotumia nguvu kamwe, wataenda watajitafakarii, ila moyoni amekubali shoo,
Mtengenezee mteja ambaye hajanunua bidhaa mazingia ya kua huru akitaka kurudi,
Sio unamwambia mteja "ukikosa utarudi".