Naomba wenye uzoefu na hizi simu za Samsung Galaxy A9(2016), C7 na C8

Naomba wenye uzoefu na hizi simu za Samsung Galaxy A9(2016), C7 na C8

Kindinga

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2015
Posts
385
Reaction score
342
Kheri ya mwaka wataalam.

Ninapata mkanganyiko kidogo kwenye kujua ipi itanifaa zaidi kati ya simu tajwa hapo juu.

Upande wa performance, ukaaji wa chaji na mambo mengine ya msingi kwa mtumiaji wa kawaida.

Nataka kununua moja kati ya hizi nimejaribu kupitia mitandaoni kuangalia ipi ni the best kwa mwenzie ila bado naona mlolongo unakuwa mkubwa na kwa vile sina uzoefu na simu za samsung napata ukakasi.

Simu ni samsung A9 2016 yenye gb 32, C7 gb 32 na C8 yenye GB 64.

Najua kuna ambao wamewahi kuzitumia hizi simu na hata wataalam na wajuvi wa mambo naombeni mnisaidie kuniambia nichukue ipi.

Nawasilisha.
 
Kioo 150k mpaka 200k vioo vya ni kioo nani njee so inafanya iwe gharama, wajinga sana
Wanazingua sana hapo japo simu zao ni nzuri zina features murua ila wanatukomoa hapo
 
Simu za Samsung version ya c ni maalum kwa china na hongkong au Taiwani kuwa makini mkuu. Ni simu zenye usumbufu wa kutosha kwa maeneo yetu.

Halafu kwanini ununue simu za kitambo?
 
Simu za Samsung version ya c ni maalum kwa china na hongkong au Taiwani kuwa makini mkuu. Ni simu zenye usumbufu wa kutosha kwa maeneo yetu.

Halafu kwanini ununue simu za kitambo?
Ahaa nilikuwa sijafaham hii, hapo nimekuelewa
 
Back
Top Bottom