Naombe kujua mtu alieambukizwa kifua kikua anaanza kuumwa baada ya muda gani?

IKWETE

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
4,057
Reaction score
694
Wakuu nilikuwa naombeni kujuzwa mtu alieambukizwa tb anaanza kuumwa baada ya muda gani.kwani mwaka wa 2011 nilimuuguuza mwanamke niekuwa nae lakin alipona kuna dalili naziona sasa sijui niliambukizwa? maana nilikohoa kwa muda wa wiki 5 pamoja na mafua na homa kidogo halafu nikapona lakini sikutumia dawa ila ya maleria. baada ya wiki moja kupita jana nimeanza kukohoa tena na mafua tena halafu natoka jasho sana sijui ndio kifua kikuu au kawaida. samahanini lakini.
 
Unapopata vijidudu vya TB(MycobacteriumTuberculosis) kawaida unapatwaga na inflammation reaction ambayo hupelekea kupata inflammation kwenye nodes(Tubercle) ambapo mwili huchukulia umepata maambukizi.Hii node inahusika na maambukizi ya TB kwenye kifua ambapo hutengeneza Primary complex.
Stage ya mwanzo ya maambukizi inakuwa haina dalili nyingi zaidi ya zile za kawaida kama mtu anapoumwa na kifua/kikohozi.Hata ukichukua kipimo huwezi kugundulika kama una maambukizi ya TB kwa kipindi hicho na huwezi kumuambukiza mtu vilevile.
Unaweza kusambaza ugonjwa huu pale ambapo hivo vijidudu vya TB vinapopata upenyo wa kutoka nje ya hio Turecle.
Baada ya miezi 3 unaweza kuona primary complex kwa xray ya mapafu.Na baada yawiki 4-6 unaweza kuchukua kipimo kinachoitwa TUBERCULIN TEST ili kugundua kamauna TB.

Kila la kheri
 
Dalili nyingine ni kutoka jasho wakati wa usiku ukiwa umelala,,,na kupata dalili za homa kuanzia mida ya alasiri mara kwa mara ....uzuri tb inatibika mradi ufuate masharti ya ile dozi japo nasikia vidonde ni vingi na unameza kwa muda mrefu...nisisahau dalili nyingine ukitembea umbali kidogo miguu inauma kwenye joint za magoti na unakosa pumzi na vichomi vya mara kwa mara
 
Tuberculin test haioneshi kama mtu ana active tb au ni kwa sababu ya exposure. Most adults in tz watareact to tuberculin test. Kuna dalili ambazo ni KUKOHOA KWA ZAIDI YA WIKI 2, HOMA, KUPUNGUA UZITO GHAFLA, KUVUJA JASHO WAKATI WA KULALA. Hizi dali kama unazo zitamfanya daktari akuandikie vipimo vya kumsupport kukuanzishia matibabu(kumbuka daktari hatibu vipimo vya maabara) na judgement ya kumuanzishia mtu dawa inategemea na hali ya mgonjwa. Kumbuka pia, kwa sera yetu kupima VVU ni lazima kwa mtu yeyote mwenye TB hivyo ujipange.! Teh. Kumbuka pia kila mtanzania ana maambukizi ya tb, tumetofautiana kwenye kuwa full blown tuberculosis, usiogope mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…