Naimani nyote mu bukheri wa afya,bila kupoteza muda mi naomba mnishauri nina diploma ya International relations and diplomacy kutoka pale chuo cha diplomasia kurasini.Then nimemaliza mwaka huu BAED pale chuo kikuu Dar es salaam(UDSM).sasa sielewi hatma yangu kiukweli sipendi kazi ya ualim hasa secondary napenda chuo lakin kwa bahati mbaya naona kazi nying za tutorial assistant wanahitaji GPA ambayo mi imepungua point 1 kufika nimekata tamaa kwakweli.Kama marafiki naombeeni ushauri career yangu iweje na ntafikiaje hayo malengo.Asanteni.