Naombeni anayejua anijuze, mfupa wangu wa mkono uliovunjika umegoma kuunga

amrir ksb

New Member
Joined
Feb 27, 2025
Posts
2
Reaction score
1
Habari zenu ndugu zangu naomba kwa anayejua anisaidie.

Mwezi uliopita nilipata ajali na kwa bahati mbaya nilivunjika mvupa wa mkono karibu na viungio katika bega sasa nina mwezi bado mfupa haujaunga zaidi nakwenda hospitali nabadilishwa P.O.P na sitaki kutia chuma nawaombeni msaada kwa anaejua wapi nitapata tiba nitapona anijuze
 
Ilibidi uweke na x-ray wataalamu waone.

Kikawaida kuunga kwa mfupa hutegemea vitu vingi ikiwemo sehemu uliyovunjika, kiungo ulichovunjika, aina ya mvunjiko, uhusika wa mishipa ya damu/mishipa ya fahamu, umri, vyakula, n.k.

Kwa mfupa uliivunjika juu sana karibu na maungio huchukua muda mrefu kuunga ukilinganisha na mvunjiko huo huo kwenye mfupa huo huo isipokuwa tu mvungiko ukawa kati, nusu ya kati - juu au chini..

Mvunjiko wa mkono karibu na bega unachangamoto sana kwenye kuunga sababu hata kufanya joint stabilization kwa hapo huwa ni ngumu. Wataalamu wa kufunga p.o.p(s) watakua wanaelewa.

Kuweka chuma inawezekana au isiwezekane kulingana na aina ya mvunjiko, thus why ilipaswa usukumie japo na ka x-ray ili wataalamu wa humu jf waweze kuona wakusaidie.
 
Habari zenu ndugu zangu naomba kwa anayejua anisaidie.

Mwezi uliopita nilipata ajali na kwa bahati mbaya nilivunjika mvupa wa mkono karibu na viungio katika bega sasa nina mwezi bado mfupa haujaunga zaidi nakwenda hospitali nabadilishwa P.O.P na sitaki kutia chuma nawaombeni msaada kwa anaejua wapi nitapata tiba nitapona anijuze

Pole sana.

Ni muhimu ukaonana na daktari bingwa wa mifupa (orthopedics surgeon) ili ushauriane naye kuhusu matibabu yako.

Samahani hospital walikushauri uwekewe chuma? Na kwa nini hutaki kuwekewa chuma?.

Mwisho, ni muhimu sana ukafanya maamuzi sahihi ya matibabu kwani kukaa na mfupa uliovunjika kwa mwezi mmoja sio salama sana.

Kila la kheri.
 
Tafuta watu wa Kanda ya ziwa huko mambo safiiiii kabisaaaa wanaunga vzr sanaaaaaa
 
Habari zenu ndugu zangu naomba kwa anayejua anisaidie.

Mwezi uliopita nilipata ajali na kwa bahati mbaya nilivunjika mvupa wa mkono karibu na viungio katika bega sasa nina mwezi bado mfupa haujaunga zaidi nakwenda hospitali nabadilishwa P.O.P na sitaki kutia chuma nawaombeni msaada kwa anaejua wapi nitapata tiba nitapona anijuze
Weka chuma. Ukiunga unatoa vyuma ukipenda.
 
Habari zenu ndugu zangu naomba kwa anayejua anisaidie.

Mwezi uliopita nilipata ajali na kwa bahati mbaya nilivunjika mvupa wa mkono karibu na viungio katika bega sasa nina mwezi bado mfupa haujaunga zaidi nakwenda hospitali nabadilishwa P.O.P na sitaki kutia chuma nawaombeni msaada kwa anaejua wapi nitapata tiba nitapona anijuze
Unaishi wapi, kama uko Kilimanjaro watalam wapo wengi tu.
 
Back
Top Bottom