Ilibidi uweke na x-ray wataalamu waone.
Kikawaida kuunga kwa mfupa hutegemea vitu vingi ikiwemo sehemu uliyovunjika, kiungo ulichovunjika, aina ya mvunjiko, uhusika wa mishipa ya damu/mishipa ya fahamu, umri, vyakula, n.k.
Kwa mfupa uliivunjika juu sana karibu na maungio huchukua muda mrefu kuunga ukilinganisha na mvunjiko huo huo kwenye mfupa huo huo isipokuwa tu mvungiko ukawa kati, nusu ya kati - juu au chini..
Mvunjiko wa mkono karibu na bega unachangamoto sana kwenye kuunga sababu hata kufanya joint stabilization kwa hapo huwa ni ngumu. Wataalamu wa kufunga p.o.p(s) watakua wanaelewa.
Kuweka chuma inawezekana au isiwezekane kulingana na aina ya mvunjiko, thus why ilipaswa usukumie japo na ka x-ray ili wataalamu wa humu jf waweze kuona wakusaidie.