Nitapenda kuchangia kama ifuatavyo:
1.Unaweza kusoma bachelor hata tatu kwa mapenzi yako na kuendana na knowledge unayotaka kupata.Epuka kusoma kama fashion.Lenga kwenye kutafuta maarifa na pia uangalie matumizi ya hizo degree.
2.Kuna namna mbalimbali za kuji position hata kama degree uliyoipata mwanzo unashindwa kuitumia. Unaweza kuitafutia linkage na masomo mengine maana dunia ya sasa inataka mtu multi-disciplinary na siyo mwenye mtizamo mmoja tu.Mfano, siku hizi kila mtu anakimbilia kusoma Law..ati kwa vile wanadhani inalipa kwa kuwaangalia mawakili wanavyotengeneza pesa! Wanasahau kuwa huko tuendako kuwa na degree ya LLB peke yake si mali kitu... unatakiwa uwe na taaluma nyingine kama Finance, management, medicine, forensic, development management,IT etc. maana specialisation ni muhimu.
Unaweza kusoma kozi fupi fupi kwenye masuala ya afya ya jamii ( public health), environment, HIV/AIDS, POVERTY,Human Rights, NGDOs etc HAYA siyo lazima uyachukulie degree bali waweza kusoma postgrad ukaichanganya na fani yako nyingine uliyoisomea ukajikuta mambo yako ni poa sana.
3. Kuhusu kutumia hizo degree kutafutia kazi, inategemea jinsi utakavyofanya maombi ya kazi na kazi husika zinataka mtu mwenye vyeti gani.Pia unashauriwa kupata uzoefu hata kama ni kwa kujitolea.Watz wengi hawajaielewa concept ya volunteersim na hapa ndipo wenzetu wazungu na wahindi au hata watu wa nchi nyingine za Africa hutupiga bao.Kujitolea bila hata kulipwa kuna faida zake a). Unapata fursa kuingia kwenye taasis na kujifunza chini ya watu mahiri na hapo hapo b). unajenga CV yako kiasi kwamba utakapokuja kuomba kazi ukiulizwa una uzoefu unaweza kujibu kwa ma confudence kuwa unayo.Watu wawe na malengo kila hatua kuanzia kusoma hadi kujiandaa kutafuta kazi.