Naombeni mmoja wenu anikopesha laki mbili

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Bwana yesu asifiwe Wana jf.Wanasema mficha maradhi kifo humuumbua,yamenifika mdogo wenu mpaka nimekuja mbele zenu kwa unyenyekevu wa Hali ya juu Sana.Mimi nina wazo la kibiashara ambalo linahitaji laki mbili nianze utekelezaji nimekwama naombeni mwenye hela aniazime namrudishia baada ya mwezi mmoja na lazima tukaandikishane polisi au kwa mwanasheria kwani nitamuwekea vitu fulani Kama Bondi.naombeni Sana mnisaidie pia Kama Kuna mtu mwenye ushauri wa bure anielekeze taasisi gani ya fedha au ofisi gani naweza kukopesheka kiasi hicho bila hati ya nyumba,kiwanja au Mali za thamani sana kwani Sina vitu hivyo.msiniangushe jamani wana jf wote Hawa kweli akosekane hata mmoja wa kuwawakilisha laki mbili tu hata sio hela nyingi Sana nazohitaji.naombeni Sana kwa sababu nimesikia anayekusaidia sio mtu unayemjua sio ndugu wa karibu Bali Ni mtu Baki nataka kuthibitisha.niko serious majamaa zangu.
 
Ukipata zaidi unigawie na mimi, huku kuna wakarimu sana! Ila mimi nikipewa sirudishi!
 
Kijijini mwenu ile 50m haijaletwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…