gsmsolution2009
Senior Member
- May 7, 2013
- 120
- 7
Mimi ni raia wa Tanzania mwenye asili ya kihindi nimekuwa nikisumbuliwa kila mara na watu wa idara ya uhamiaji kwa mfano wiki iliyopita wakati natembea akatokea mtu wa uhamiaji akanivuta mkono ghafla nilivyogoma kusimama kwa vile sikumjua ni nani akanitolea kitambulisho chake na kuniuliza maswali baada ya kumjibu maswali yote akaniuliza kitambulisho chochote nikamwambia nimekiacha nyumbani akanijibu kwa sababu niligoma kusimama mpaka anionyeshe kitambulisho kwa hiyo na yeye ananiaumbua tungozane mpaka nyumbani nikamuonyeshe vitambulisho kwa vile nilikuwa nimevaa begi yenye vitu vyenye thamani na duka letu lilikuwa kama hatua kumi jirani nikamwomba niache begi dukani akagoma na kunivuta mkono kwa nguvu niongozane nae mpaka watu wakajazana na kuanza kuwasema waache uonevu ndio wakaniachia na leo hii nilikamatwa tena na idara ya uhamiaji na watu wengine kabla ya kuanza kuwajibu nikamwomba kitambulisho akanionyesha nikaanza kumjibu akaniomba kitambulisho nikamwonyesha kadi ya uraia akaniambia hawezi kuamini hiyo kadi naweza nikawa nimetengeneza kiujanja akaniambia kwa vile nilifanya kosa la kumuuliza kitambulisho kwa hiyo na yeye atanisumbua kunipeleka ofisini kwao mpaka niwaonyeshe kitambulisho watakachoamini ikawa sina jinsi nikakubaliana naye kwenda ofisini tulivyofika nusu njia akawa ananiambia nisifanye kosa la kuwaomba kitambulisho tena na kuniachia niondoke. Hapo nimeandika kuhusu mara mbili ila huwa nasumbuliwa kila mara naombeni msaada wenu nini cha kufanya