Naombeni mniambie jinsi ya kupeleka malalamiko idara ya uhamiaji

gsmsolution2009

Senior Member
Joined
May 7, 2013
Posts
120
Reaction score
7
Mimi ni raia wa Tanzania mwenye asili ya kihindi nimekuwa nikisumbuliwa kila mara na watu wa idara ya uhamiaji kwa mfano wiki iliyopita wakati natembea akatokea mtu wa uhamiaji akanivuta mkono ghafla nilivyogoma kusimama kwa vile sikumjua ni nani akanitolea kitambulisho chake na kuniuliza maswali baada ya kumjibu maswali yote akaniuliza kitambulisho chochote nikamwambia nimekiacha nyumbani akanijibu kwa sababu niligoma kusimama mpaka anionyeshe kitambulisho kwa hiyo na yeye ananiaumbua tungozane mpaka nyumbani nikamuonyeshe vitambulisho kwa vile nilikuwa nimevaa begi yenye vitu vyenye thamani na duka letu lilikuwa kama hatua kumi jirani nikamwomba niache begi dukani akagoma na kunivuta mkono kwa nguvu niongozane nae mpaka watu wakajazana na kuanza kuwasema waache uonevu ndio wakaniachia na leo hii nilikamatwa tena na idara ya uhamiaji na watu wengine kabla ya kuanza kuwajibu nikamwomba kitambulisho akanionyesha nikaanza kumjibu akaniomba kitambulisho nikamwonyesha kadi ya uraia akaniambia hawezi kuamini hiyo kadi naweza nikawa nimetengeneza kiujanja akaniambia kwa vile nilifanya kosa la kumuuliza kitambulisho kwa hiyo na yeye atanisumbua kunipeleka ofisini kwao mpaka niwaonyeshe kitambulisho watakachoamini ikawa sina jinsi nikakubaliana naye kwenda ofisini tulivyofika nusu njia akawa ananiambia nisifanye kosa la kuwaomba kitambulisho tena na kuniachia niondoke. Hapo nimeandika kuhusu mara mbili ila huwa nasumbuliwa kila mara naombeni msaada wenu nini cha kufanya
 
Mhh!labda walikuwa wanataka rushwa!but ushauri wangu kila atakaekufata akidai ye ni uhamiaji muombe kitambulisho na uangalie kama ni chake na ni halali.maana wanaweza hata wakatengeneza vitambulisho feki na wanavitumia kutapeli wale wahamiaji wasio na kibali but Kama wewe una vibali vyote hali vya kuishi nchini usitishike wala usiwe na shaka.hakikisha mda wote unavyo ili wakitokea wasikusumbue na wasikutapeli.uhamiaji halisi hawafanyi hivyo,ukiwaonyesha vibali na wakiona ni halali wanakuacha tu kwa amani uendelee na yako but haoni makanjanja wa mjini.kama ni kweli uhamiaji kwanini wasikufikishe ofisi zao na wakushushe njiani?kwanini wakukataze kuuliza vitambulisho vyao wakati ni haki yako?kuwa makini kaka ikiwezekana nenda ofisi za uhamiaji uwajulishe hili na upate maelezo zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…