nilipatwa na pressure 190 kwa 107.na nilikuwa na proteins kibao kwenye mkojo
Hii kweli ni Pre - Eclampsia, ambayo ni ugonjwa unaohusisha pressure ya kupanda pamoja na protein kwenye mkojo kwa mama mjamzito
baada ya wiki ya ishirini ya ujauzito. Kama ni pressure peke yake ndio iko juu bila protein kwenye mkojo, hii huitwa '
gestational hypertension'. Kama utakuwa na pressure kabla ya wiki ya ishirini ya ujauzito hii huwa ni
chronic hypertension (hypertension ambayo mtu anayo siku zote kabla hajawa mjamzito either akijua au asipojua kwani hatuna kawaida ya kupima afya. Endapo hii chronic hypertension itaambatana na protein kwenye mkojo baada ya wiki ya ishirini ya ujauzito sasa itaitwa
chronic hypertension with superimposed pre-eclampsia.
Ma Dr wakashauri na nikainduziwa,namshukuru MUNGU nilijifungua salama.
Tiba ya pre-eclampsia na hasa kama iko severe [dalili za severe pre-eclampsia ni BP ya 160/110, protein kwenye mkojo ya 3+, maumivu kwenye chembe ya moyo, kichwa kuuma sana, kutoona vizuri (blurring of vision)]au mama yuko term ni delivery. Kabla hujafika term na pre-eclampsia sio severe unaweza ukatumia dawa za kushusha pressure na kama pressure itakuwa controlled unaweza kusubiri mtoto akakua na ukajifungua salama.
napenda kujua sababu za kupatwa ha hii kitu
Kwanza nieleze dalili za pre-eclampsia hutokeaje, mechanism iko complex kidogo lakini nitajaribu kurahisisha ili hata muhasibu aweze kuelewa.
pre-eclampsia inasemekana kusababishwa na mama mjamzito kuwa exposude kwenye chorionic villi ambazo ni tissue za placenta upande wa mtoto zitumikazo kupeleka virutubisho na hewa kwa mtoto na hizi huwa zina chembe hai au uhusiano na upande wa baba (partenal side), kwa hiyo mwili wa mama utaziona hizi kama kitu kigeni (foreign tissues) kwa kuwa zina uhusiano na baba na si sehemu ya mwili wa mama na hivyo mwili wa mama kutoa kinga (antibodies) kwa ajili ya kuzishambulia hizo foreign tissue (antigens) na hivyo husababisha utengenezwaji wa muungano wa hizi antibodies na antigen (antibody-antigen complexes). Hizi complexes husafiri mwilini na kwenda kuumiza baadhi ya viungo vya mwili ikiwemo chujio la figo na hivyo kusababisha lile chujio kupitisha hata molecules kubwa kama protein (hasa albumine) ambazo kikawaida hazipiti kwenye chujio lile na mama kupitisha protein kwenye mkojo (proteinuria).
Protein zinazunguka pamoja na damu kwenye mishipa ya damu, na kazi yake ni kuhakikisha damu pamoja na majimaji yake (serum) inabaki kwenye mishipa yake (yaani haiendi kwenye nyama za mwili - extravascular space). Protein zinapopungua kwa kutoka mwilini kwa njia ya mkojo, ile pressure kwenye damu (oncotic pressure) ya kufanya majimaji ya kwenye damu yabaki kwenye mishipa yake hupungua na hivyo maji huanza kuhama kutoka kwenye mishipa ya damu na kwenye kwenye nyama za mwili (extravascular space) na mama mwenye pre-eclampsia ataonekana amevinda mwili (oedema) kwa ajili ya hayo maji yanayotoka kwenye mishipa ya damu.
Majimaji haya yanapopungua kutoka kwenye mishipa ya damu kwenda nje, mwili utasense kwamba kuna upungufu wa maji kwa maana hiyo ili damu ya kutosha iweze kuzunguswa mwili inabidi moyo ufanye kazi ya ziada ya kusukuma damu kwa kasi zaidi ili ile kidogo iliyobaki iweze kuzunguka mwili na kupeleka damu sehemu mbali mbali za mwili. Usukumaji damu kwa kasi ndio huleta pressure (hypertension).
Sababu hasa ya pre-eclampsia haijajulikana lakini hutokea zaidi kwa:
1. ujauzito wa kwanza,
hii ni kwa sababu ya exposure ya chorionic villi kwa mara ya kwanza, kwenye mimba zinazofuata mwili wa mama utakuwa umezizoea hizo chorionic villi na hivyo hauta-react kusababisha pre-eclampsia kama nilivyoeleza juu. Inapotokea mama amebadilisha mume, au amezaa na mwanaume mwingine, uwezekanao wa kupata pre-eclampsia ni mkubwa hata kama alishazaa kabla kwa sababu mwili wake sasa utakuwa exposed kwa chorionic villi mpya.
Kwa hiyo change of husband or partner may predispose to pre-eclampsia.
2. Mama mwenye watoto mapacha au wale wenye mimba zabibu (hydatidform mole) wana uwezekano pia wa kupata pre-eclampsia kwa sababu wanakuwa na chorionic villi nyingi zaidi (superabandance of chorionic villi).
3. Kama mama ana ugonjwa wa mishipa ya damu (vascular disease) kama atherosclerosis.
4. Kama mama yuko genetically predisposed to hypertension in pregnancy. Ndio maana si kina mama wote watapata pre-eclampsia pamoja na kwamba wote wanakuwa exposed to chorionic villi, wengi ni wale ambao genetically wako predisposed. Ndio maana mtu mwenye mama au dada aliyewahi kupata pre-eclampsia ana hatari zaidi ya yeye ya kupata pre-eclampsia.
5. Uzito mkubwa (obesity) pia huchangia. Kwa sababu ya mafuta kwenye mishipa ya damu, huongeza uwezekano wa pressure.
6. Mtu mwenye magonjwa ya figo, kisukari na rheumatoid arthritis.
Kwa sababu chanzo hasa hakijulikana, njia za kuzuia pia ni ngumu, labda tu ile ya kuhakikisha unazaa na mume mmoja itakupunguzia uwezekano, punguza unene, kama ni mgojwa wa kisukari hakikisha kimekuwa controlled, kama kuna historia ya pre-eclampsia kwenye ukoo hakikisha unawahi hospitali na ufuatiliewe kwa ukaribu unapokuwa mjamzimto. Vinginevyo hakuna chanjo ya pre-eclampsia.
any way nina appointment na Dr wa Figo ili anipime kama pressure iliaffect figokuna uhusiano gani?
Kuna uhusiano mkubwa, ugonjwa wa figo unaweza kuleta pressure lakini pressure pia huweza kuleta ugonjwa wa figo, ndio maana wagonjwa wote wa pre-eclampsia lazima wapimwe utendaji kazi wa figo zao (renal function tests).
Natanguliza shukurani zangu
Karibu sana, natumaini nimekusaidia.