Naombeni mnisamehe bure, mtanzania mwenzenu

Junior Rutashoborwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2019
Posts
228
Reaction score
210
Kukosea ni vibaya ila kutokuomba msamaha ni vibaya zaidi.

Napiga magoti mbele zenu watanzania wenzangu naombeni mnisamehe.

Sikufanya hivyo kwa makusudi sema nilisahau kuwa nchi ambayo babu yangu alizaliwa bado ni ulimwengu wa tatu.

Katika maisha yangu tangu nimezaliwa hapa Manhattan, NYC. sijawahi kushuhudia kukata kwa umeme. Nilikuwa nasikia tu kwenye simulizi za kale kuwa kuna watu wanaweza ishi bila mwanga wa umeme, nilikuwa nashangaa sana.

Naogopa giza sana, na ndio maana natamani kwenye kabuli langu wafunge taa ili siku nikiamka nisikutane na giza.

Rafiki yangu Naseeb, aliniambia TZ umeme kukata pale mtu anapoishiwa na voucher (Nyie mnaita LUKU) . Kwa sababu sipendi giza niliamua kumuagiza Cousin Rhurenberg Kamugisha aninunulie luku ya mwaka mzima...

Kumbe NVR worth less than the amount I gave to him.

Najuta kwa kusababishia nchi hasara ya pesa hasahasa kwa watanzania wenye vipato vya chini.

Nisameheni bure sikujua.

Samahani Tz kiwango cha chini cha pesa nazoruhusiwa kutoa bank ni Tsh. Ngapi? Nahofia watu kukosa huduma za kibenki siku nikija Tz.

Baada ya Wiki nili naweza kuwa Dar Es Salaam ila nitakuwa nalala visiwani Zanzibar.
 
Kumbe ni wewe! Maana nilisikia ni Mhaya fulani ndio katuletea shida sisi wanunuzi wa umeme wa buku! (Buku ni <$0.5)
 
Katika maisha yangu tangu nimezaliwa hapa Manhattan, NYC. sijawahi kushuhudia kukata kwa umeme. Nilikuwa nasikia tu kwenye simulizi za kale kuwa kuna watu wanaweza ishi bila mwanga wa umeme, nilikuwa nashangaa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…