Naombeni msaada juu ya Sheria hii ya Usalama Barabani!

Naombeni msaada juu ya Sheria hii ya Usalama Barabani!

8691jakigili

Senior Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
179
Reaction score
67
Moja ya sheria za usalama wa barabarani inasema: "Usiendeshe gari huku umelewa." Leo, nikiwa ndani ya daladala narejea nyumbani kutoka katika mihangaiko ya maisha nimepita karibu na baa kubwa hapa Arusha na kuona sehemu zote za kuegeshea magari zikiwa zimejaa magari na watu wanakunywa pombe! Sasa, hiyo sheria inafanya kazi namna gani? Kwa mfano, ikiwa mimi ni askari wa usalama wa barabarani je, nina haki ya kwenda pale baa na kuyazuia yasiendeshwe na walevi hao ili kuzuia ajali ambazo zinaweza kusababishwa na ulevi?

Wanajamii Wanasheria nisaidieni kutatua utata huu wa sheria!!
 
Naam! Kadhalika si wote waendao baa na magari yao hawanywi kilevi!!!
 
Sheria inasema usiendeshe gari ukiwa umelewa na siyo usiende baa na gari lako, hivi ni vitu viwili tofauti. Sheria inambana awapo barabarani akiwa amelewa na siyo kwenye baa. Unajuwaje labda anadereva wake atakaemwendesha baada ya kulewa. Kwa hiyo wewe unataka watu wazuiwe kwenda baa na magari?
 
Sheria inazuia kuendesha gari ukiwa umelewa na haizuii kunywa pombe ukiwa na gari ndo maana wameweka kiwango kuwa ukikamatwa na alcohol content ya zaidi ya 0.5 kwa kipimo cha breathlyzer ambayo approximatelly kwa vibia vya chupa za kijani ni 3 unakuwa umetenda kosa
 
Kimsingi polisi wangeweza wangezuia kila mlevi asiendeshe gari. Ni suluhisho zuri kumzuia mtu akiwa baa, ikiwa kuna uhakika wa kulewa.
 
Back
Top Bottom