Moja ya sheria za usalama wa barabarani inasema: "Usiendeshe gari huku umelewa." Leo, nikiwa ndani ya daladala narejea nyumbani kutoka katika mihangaiko ya maisha nimepita karibu na baa kubwa hapa Arusha na kuona sehemu zote za kuegeshea magari zikiwa zimejaa magari na watu wanakunywa pombe! Sasa, hiyo sheria inafanya kazi namna gani? Kwa mfano, ikiwa mimi ni askari wa usalama wa barabarani je, nina haki ya kwenda pale baa na kuyazuia yasiendeshwe na walevi hao ili kuzuia ajali ambazo zinaweza kusababishwa na ulevi?
Wanajamii Wanasheria nisaidieni kutatua utata huu wa sheria!!