Habari za majukumu wanajukwaa. Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.
Nina ndugu yangu kaenda marekani, Texas. Sasa kanambia anataka anitumie pesa kwa njia ya Western union. Hii njia ni ngeni kwangu, sijui chochote. Naombeni wadau mnisaidie. [emoji117]Je natakiwa kufuata hatua zipi?
[emoji117]Je inatolewa kwenye mabenk au mawakala wa kawaida?
[emoji117]kama inapatikana benki, ni benk gani inatolewa hii huduma?
Naombeni mnieleweshe wadau nipate pa kuanzia. Natanguliza shukrani kwenu mtakaokuwa na moyo wa kunielewesha. Ahsanteni
sent using super amoled display
Ahsante sana. Je kuna viambatanisho vyovyote natakiwa kumtumia yeye kule? Mfano my account number na taarifa nyingine zozote kutoka huku ndio anitumie hiyo pesa?Wala usiwe na wasiwasi, hakikisha huyo ndugu yako ana majina yako halisi kama yanavyoonekana kweney kitambulkisho chako kama lesseni, pasipoti au kitambulisho cha taifa (Chenye sahihi). Akishakutumia mpunga, atakutumia namba kama kumi hivi, hizto utazijaza siku unaenda kutoa pesa zako.
Mabenki mengi tu yanatoa huduma za western union, kwa uchache ni haya Benki ya Posta, KCB, Diamond trust na nyingine nyingi.
Ahsante sana mdau. Na vipi kuhusu viambatanisho vyovyote toka kwangu kama my account number na taarifa zangu?Hii ni moja na njia za zamani sana za kutumiwa pesa. Sasa akishakutumia atapewa control number nafikiri inaitwa MTN atakuambia na huwa kuna namba ya siri utakuaambia ukienda mahali pa kutolea ambapo hapa njini nafikiri benki ya posta, DTB na boa ndio wakala ninaowafahamu. Nenda na kitambulisho utapewa form utajaza utatoa hela unikumbuke kwenye ufalme wako
Ahsante sana. Je kuna viambatanisho vyovyote natakiwa kumtumia yeye kule? Mfano my account number na taarifa nyingine zozote kutoka huku ndio anitumie hiyo pesa?
sent using [emoji85]
Kwahiyo kumbe inawezekana pia kutumiwa kwa njia ya account ya benk. Hii njia ipoje piaHauhitaji kumtumia account number yako ya benki, vinginevyo iwe anakuingizia pesa moja kwa moja kwenye account yako.
Unawezamtumia nakala ya kitambulisho chako na anwani yako.
Hakuna account wala nini.. We mpe ndugu yako majina yaliyopo kwenye kitambulisho na usikosee herufi hata moja!!Ahsante sana. Je kuna viambatanisho vyovyote natakiwa kumtumia yeye kule? Mfano my account number na taarifa nyingine zozote kutoka huku ndio anitumie hiyo pesa?
sent using [emoji85]
Kwahiyo kumbe inawezekana pia kutumiwa kwa njia ya account ya benk. Hii njia ipoje pia
sent using [emoji85]
MTCN
Mwambie akutumie kwa Skrill. Hakikisha account yako ya bank ipo connected na hiinhuduma
Be blessedUnaenda bank yyte yenye huduma ya Western Union
Unatumia kitambulisho Cha mpiga kura,Cha uraia ama Cha kazi
Hakikisha anaekutumia ameandika majina yako sahihi na zile pin(password) anakupa
Unatoa bila matatizo..bank wataiconvert into tshs
Sent using Jamii Forums mobile app