Isosorbidmononitrate ni dawa inayotumika kutibu matatizo ya moyo
ANGINA PECTORIS
Angina pectoris ni ugonjwa wa moyo unaosababisha kukaza kwa muscle ya moyo ambayo hupelekea kupungua kwa msukumo wa damu.
Dalili zake ni maumivu ya kifua ambayo yanasambaa mpaka kwenye mkono na shingo,kupumua kwa uzito na uchovu.
Hii dawa inasaidia kufanya smooth muscles kurelax kwa kutengeneza NO (nitrogen oxide) na cGMP.
Inaupunguzia moyo uzito wa kufanya kazi ya kusukuma damu ambayo haina oksygen ya kutosha na hatimae kupunguza maumivu.
Side effects za dawa hii ni kwamba unakuwa dose dependent,yaani baada ya muda unakuwa unahitaji uongeze dozi iwe juu kwasababu ya chini haifanyi kazi.
Unaweza kuepuka hali hii kwa kuwa na nitrate free intervall ya masaa 8-12 kila siku na kuepuka kula kutumia dawa frequently haswa long acting nitrates.
Wengi wanapatwa na maumivu ya kichwa mwanzoni mwa matumizi lakini hali hio inaondoka baada ya wiki za mwanzo.Inaweza kusababisha kushuka kwa presha na kuongezeka kwa mapigo ya moyo.
NI MUHIMU SANA ukitumia dawa hii usichanganye na
- VIAGRA(sildenafil) kwa sababu inasababisha kushuka kwa presha na sideeffect inayopelekea heart attack.
- Haipaswi kuchanganywa na dawa nyingine kama (ACE-Inhibitors,calsium antagonists,Betablocks,Diureticum) hizo ni dawa za presha na zinatumika pia kutibu moyo
- Tricyclic antidepressants ambayo ni dawa ya depression na pombe.Mchanganyiko na dawa hizo hupelekea kushuka sana kwa presha.
- Mchanganyiko na NSAID´s(non-steroid antiinflammatory drugs kama acetylsalicylic acid(asprin),ibuprofen,dispril,diclofenac) husababisha dawa kutofanya kazi ipasavyo.
- Ukitaka kuacha hii dawa uache taratibu(step down)