Katika hali ya kawaida muajiri wenu wa mwanzo alitakiwa awaeleze hatima ya ajira zenu. Kama zinaendelea then lazima kuwe na ushahidi kwamba terms zitakuwa ni zilezile na hiyo mara nyingi huwa ni kwa maandishi. La kama Ajira mpya inaanza, mwajiri wa zamani lazima amaliziane na nyinyi labda kama kwenye mkataba wao wa manunuzi unasema kuwa malipo yenu yatalipwa na mwajiri mpya.Kwa mfano mtu anafanya kazi na kampuni fulani, baada ya muda hiyo kampuni inatolewa kutoka kwa mwendeshaji moja na kupewa mwingine na inabadilishwa jina. Mwendeshaji mpya anaamua kutoa mikataba upya tofauti na ile ya kampuni ya kampuni ya kwanza.
Swali ni kwamba: wale wafanyakazi ambo mikataba yao ya nyuma ambayo bado haijaisha, watatakiwa kulipwa kwanza alafu ndo wachukue mikataba ya kampuni mpya ukizingatia ya kwamba mkataba mpya unawarudisha katika probation period?
Naombeni msaada wenu hapo
Katika hali ya kawaida muajiri wenu wa mwanzo alitakiwa awaeleze hatima ya ajira zenu. Kama zinaendelea then lazima kuwe na ushahidi kwamba terms zitakuwa ni zilezile na hiyo mara nyingi huwa ni kwa maandishi. La kama Ajira mpya inaanza, mwajiri wa zamani lazima amaliziane na nyinyi labda kama kwenye mkataba wao wa manunuzi unasema kuwa malipo yenu yatalipwa na mwajiri mpya.
Hivyo basi usisaini mkataba mpya kabla ya ule wa mwanzo kuisha. Vinginevyo tafuta mwanasheria ambaye ataongea nao hao waajiri ili uweke mambo yako sawa hapa mwanzo. Kwa vyovyote vile ukisaini mkataba huu mpya ule wa mwanzo umeukana tayari na hautakuwa na nguvu kisheria tena. Kama huu wa sasa una maslahi basi we anguka tu. Lakini ujue ule wa mwanzo unakufa automatically. Na inavyoonyesha hapa huyo mwajiri wenu wa mwanzo amewauza na nyie vinginevyo angevunja mkataba wenu kabla hajauza hiyo kampuni. Lakini uwe makini katika kulijadili hili unaweza pia ukafukuzwa kazi kwa kigezo kuwa hawakuhitaji. Hivyo wanavunja huo mkataba wako wa awali na kuachana nawe kabisa.