Naombeni msaada kwa wale wafugaji wa kuku

Naombeni msaada kwa wale wafugaji wa kuku

Joined
Sep 15, 2017
Posts
18
Reaction score
10
Habari jamani, nduguzangu poleni na majukukumu, naomba msaada wenu kuku wangu wana shida moja, kwenye kutotoa ukute kuku ana mayai 12 lakini anatotoa machache Sana naombeni msaada wenu juu ya hili.
 
Uwezo wa kuku kuatamia unategemea na ukubwa wa umbo lake, kama kuku wako ana umbo dogo unawezamwekea mayai machache kama 7 au nane.Kama ataendelea kutotoa machache zaidi jaribu kutazama uhifadhi wa mayai hayo
 
Jaribu kubadili mbegu, huenda uzao wao umekua sana sasa wanakua ni kama kaka na dada
 
Angalia chanzo cha mayai yako mayai yanayoweza kuangulika vyema yasiwe yamekaa siku nyingi(vizuri chini ya siku 10),yasiwe yamechafuliwa kinyesi cha kuku,yahifadhiwe sehemu isiyokua na joto na yenye mzunguko wa hewa,hifadhi sehemu ya iliyochongoka ikiangalia chini,usichague mayai makubwa sana kwa ajili ya kutamia tumia ya size ya kati
 
Hapa nimepata somo,nilikuwa naweka mayai yaliozidi siku 10 matokeo yake mengi hayakutotolewa,kumbe ni chini ya siku 10..
 
Back
Top Bottom