Za asubuhi nyote.
Naombeni msaada kidogo wa kupatiwa maeneo ambayo kuna wakulima wengi wenye kulima mazao ya biashara. Na wakulima wenyewe wanauza kwa vikundi au wanauzia makampuni moja kwa moja. Mazao yenyewe yawe tofauti na pamba na korosho ambayo yanaukiritimba zaidi na siasa ndani yake.
Itakuwa vizuri nikipata jina la wilaya pamoja na mkoa ili niweze pia kwenda na kujiridhisha sababu kuna mradi nataka kufungua katika maeneo hayo.
Ikiwezekana naomba na majina ya makampuni au mawasiliano yao.
Natanguliza shukrani.