Naombeni msaada wa haraka jamani, vinginevyo naumbuka

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
14,540
Reaction score
30,875
Jamani nipo hapa magomeni usalama kisuma bar nimekuja na Dada zangu wametoka mpwayungu dodoma nikawaambia waagize vinywaji mm naenda toilet.

Sasa chakushangaza nimetoka maliwato Ile nafika wote wawili wameagiza savanna nane yaani kila mtu nne nne. Nimepigwa na butwaa maana hivi vinywaji imported hapa kisuma ni 5000 namm nimekuja na hela ya eagle na pliziner tu vinginevyo hii ni kesi.

Sasa nimekuja haraka humu jukwani center of intelligence mnipe ushauri wa haraka vinginevyo tutaitwa vibaka hapa.
 
Vile ambavyo wamefungua lipia mkuu, vile ambavyo bado waambie warudishe. Isitoshe kama ni dada zako kweli huwezi kuwaonea aibu, utawapa makavu uwezo wako mfukoni ili waone mnafanyaje, maybe wao wako vizuri.
Ushamba tu umewasumbua na hawana hata Mia wapo wapo tu ni dada zangu wa damu
 
Unataka ushauri au mchnago. Oh umesema ushauri.
Wambie wachangie
 
Nenda tena chooni,afu pita hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…