Naombeni msaada wa haraka wa kuelimishwa kuhusu HOMA YA MANJANO(Yellow Fever)

bachelor sugu

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
2,689
Reaction score
3,646
Jambo Tanzania,

Naombeni msaada wa haraka wa kuelimishwa kuhusu HOMA YA MANJANO(Yellow Fever)

Wakuu ktk pitapita zangu kwenye taasisi moja ya kutoa elimu(Shule)Nimekutana na mtoto mmoja ambaye ana dalili zifuatazo:

=Macho yake ni ya njano
=Pia kucha zake nazo zinaelekea kuwa na rangi ya njano
=Katumbo kake kama kakubwa kidogo japo inasadikika mtoto huyo anapenda sana kula

Hizo ni baadhi ya dalili ambazo nimeziona Nimeingiwa na hofu baada ya kusikia watu wakiisema ni homa ya manjano japo sio madaktari but nikavuta picha kuhusiana na ile condition kuwa ili uweze kwenda nje ya nchi lazima upate ICV(International Certificate of Vaccination)baada ya kuchanjwa chanjo yake sasa nikahisi ni ugonjwa hatari.

Mara ya kwanza nilikutana na huyu mtoto mtaani nikapatwa na shauku ya kumfuatilia ili nijaribu kumsaidia kwa kadri ndipo nilipoelekezwa kuwa ni mwanafunzi wa darasa II ktk shule moja hv.

Cha ajabu nimefika pale na kukutana na MWL Mkuu na kuzungumza nae binafsi nimeshangaa coz wao hawana wasiwasi na ugonjwa huo na wanamtambua huyo mtoto,kiukweli nikajiuliza je km ndio hiyo yellow fever hawezi kuwaambukiza kwa hao watoto wengine wanaosoma nae??

Tafadhali wajuvi wa tiba naombeni msaada hasa elimu kuhusu hii YELLOW FEVER.Zifuatazo chini ni Picha za hako katoto.

Sincerely,bachelor Sugu.
 
Usually hii hali ya jaundice huwa inahusiana na ini yaani liver. Mpeleke afanyiwe kipimo cha hepatitis.
 
Hospitali atapelekwa nasubiria niwafahamu walezi wake maana anaishi na bibi tu.Pia nimemuachia jukumu la kuwaita hao walezi.
Mpeleke hospital hapa utamkutana na vijana wa lumumba watakuzingua tu

Swissme
 
Yellow fever ni haemorrhagic viral infection inayoenezwa na mbu. Virus hushambulia ini na dalili zake ni pamoja na kuwa na mwili wa njano, mkojo wa njano, kuumwa kichwa, kutapika matapishi ya njano na kuishiwa nguvu pamoja na kuumwa muscles.
 
Ok vizuri mkuu bt je ini likipata shida huwa linapona?
 
Aisee yawezekana kuna ukweli ktk hili Mkuu maana pia katika kuendelea kudodosa kwangu huku pia kuna mtu pia amesema kitu hiki kuwa inasadikika huyu mtoto ana sickle cell.
Nimeshuhudia kabisa macho ya mtoto mwenye sickle cell yakiwa hivyo. Zamani kulikuwa na program ya kuwatibu bure watoto wenye sickle cell. Lakini baadaye nasikia hiyo huduma iliondolewa.

Kama mzazi hana uwezo, matibabu yanaweza kusumbua.
 
Hata sasa sickle cell kwa mtoto au mtu asiekuwa na uwezo anatibiwa bure kabisa.
Kuna watu wa ustawi wa jamii wanathibitisha kama mgonjwa hana uwezo kisha anapata tiba bure.
 
Dah wakuu nimeingiwa na ganzi baada ya kupata taarifa hapa kutoka kwa kaka wa haka katoto ambaye ni mama zao wanazaliwa pamoja ila bahati mbaya wote walishafariki so watoto hawa wote wanalelewa na Bibi.

Habari ni kuwa huyu mtoto anasumbuliwa na sickle cell anaemia na ameshalazwa sana hospitali ya wilaya na hii hali aliyonayo kiufupi wameshaizoea.

Labda tu niombe msaada wa mawazo tu namna ya kuweza kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…