Naombeni msaada wa hii ndoto yangu inayojirudia rudia

Naombeni msaada wa hii ndoto yangu inayojirudia rudia

Mel James

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2015
Posts
356
Reaction score
290
Habari zenu wakuu!!
Mara nyingi nimekuwa nikiota ndoto moja mda mrefu sana na ndoto inayonitesa sana. Naweza kukaa week mbil au moja ikajurudia ila haipiti mwezi sijaota. Nimekuwa nikiota na kula bablishi kubwa sana mdomoni ambayo inanitesa sana kuitoa hadi ndoto inaisha iyo bablishi inanata sana kwenye meno na navyoitoa haishi mdomoni hadi nashtuka na meno yanauma sana. Mda mwingne navyoangaika kuitoa nahisi nashindwa kupumua. Kwa mtu anayejua ndoto naomba msaada tafadhali niweze kuepukana na hili.
 
Badili mawazo yako... Mara nyingi ndoto ni matokeo ya kile unachokifikiria sana kabla ya kulala...
 
Mhhhh.....aiseee ebu jalbu kusali kabla ujalala lkn io ndoto yako io....lazma kuna kitu inamaanisha..
 
Kweli hapo ni sala tu ukifanya hivyo hautaota ndoto mbaya. Kujua ina maanisha nini ngoja waje
 
Sali kijana, kuna vitu utakuwa unalishwa usiku.

mshana jr anaweza kutupa tafsiri
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ni michezo ya wanga wanakulisha ngozi za wanyama most likely fisi,cha kufanya lala na mfupa wa kitimoto au pakaza mafuta yake kitandani au ukiweza jipake mwilini wakati wa kulala
 
Hiyo ni michezo ya wanga wanakulisha ngozi za wanyama most likely fisi,cha kufanya lala na mfupa wa kitimoto au pakaza mafuta yake kitandani au ukiweza jipake mwilini wakati wa kulala

Mshana samahani me na ndoto uwa naota mara nyingine natoa manyoya mdomoni ya kuku yaweza kuwa sawa na hiyo? Kama ni sawa na hiyo ntafanyaje kumjua mbaya wangu?
 
Habari zenu wakuu!!
Mara nyingi nimekuwa nikiota ndoto moja mda mrefu sana na ndoto inayonitesa sana. Naweza kukaa week mbil au moja ikajurudia ila haipiti mwezi sijaota. Nimekuwa nikiota na kula bablishi kubwa sana mdomoni ambayo inanitesa sana kuitoa hadi ndoto inaisha iyo bablishi inanata sana kwenye meno na navyoitoa haishi mdomoni hadi nashtuka na meno yanauma sana. Mda mwingne navyoangaika kuitoa nahisi nashindwa kupumua. Kwa mtu anayejua ndoto naomba msaada tafadhali niweze kuepukana na hili.

....kuna kitabu fulani kina kava jeusi.....kitabu hiki kilimshangaza mfalme wetu baaada ya kusaidia mambo mengi...jaribu uwe unakiweka chini ya mto wakati wa kulala......manake waweza kuwa mvivu kukisoma.......
 
Mkuu kuweka kitabu hata kama ni cha Mungu chini ya mto siyo suluhusho,na kama huwa unafanya hivyo unakosea.kitabu hicho hakikutengenezwa ili kiwekwe chini ya mto,unatakiwa yaliyoandikwa ktk kitabu hicho yakae katika moyo wako na si kichwani chako(kuna tofauti neno la Mungu likikaa kichwani mwako na moyoni mwako).Ukiyaishi hayo,wala hakuna atakayekusumbua kama ni mchawi au nguvu yoyte mbaya.
 
Habari ndugu.

Mimi si mtaalamu sana lakini kwangu ndoto zina maana kubwa sana.

kwanza kabisa kwa manufaa ya wote, Ndoto zinatokana na sababu tatu ninazozijua.
1. Mawazo yako
2. Mawazo/Ujumbe kutoka kwa Mungu
3. Shetani.

Kama ndoto hii ingekua inatokana na mawazo yako yanayojirudia mara kwa mara kipindi ukiwa macho basi usingeota jinsi ulivyoota.

Ndoto yako imekuja kwa mafumbo. Mungu uzungumza kwa mafumbo, na kwa kuwa ndoto yako inajirudia rudia basi jua ilo linalokutokea kwenye ndoto liko karibu kutokea kwenye mwili yaani ualisia.

KAMA WEWE NI MSOMAJI WA BIBLIA NADHANI UNAKUMBUKA NDOTO YA WALE WAFUNGWA WALIOKUA NA YUSUFU GEREZANI.........Ndoto zao zilikua na mafumbo na hata farao aliota anaona ng'ombe saba ambao walimaanisha miaka saba.......

Kinywa tafsiri ya kiroho ni macho na masikio nikimaanisha nini basi unatumia kinywa chako kula sio? Chakula kinameng'enywa na meno halafu unameza sasa katika malisho ya kiroho unayapata kwa kuona na kusikia. kwa kuona miujiza mtu uamini na kwa kusikia neno la Mungu hata Imani ujengeka.

sasa turudi kwenye ndoto yako, bublish uliyokua nayo mdomoni ilikua kubwa na ilikua ikufanya kuwa uncomfortable. Kwa ufahamu kidogo nilionao basi ni kwa shetani atajaribu kukulisha vitu ambavyo ni viovu na Mungu anajaribu kukupata warning mapema. Kumbuka kuna wakati hadi ilikua unakosa pumzi.....pumzi ni uhai inamaana utakuta na mafundisho au mapokeo ya kuzimu ambayo yatakua so uncomfortable to you kiasi cha kubana uhai wako.

Jaribu kusoma Habari za Yusufu katika kitabu cha Mwanzo, Soma pia ndoto za Daniel, na hata Ezekiel. Namwomba Mungu akulinde na akuepushe na mpango wowote wa shetani katika Maisha yako. Mungu aanakupenda na kukujali ndio maana umeota hiyo ndoto. Ubarikiwe sana.
 
Habari zenu wakuu!!
Mara nyingi nimekuwa nikiota ndoto moja mda mrefu sana na ndoto inayonitesa sana. Naweza kukaa week mbil au moja ikajurudia ila haipiti mwezi sijaota. Nimekuwa nikiota na kula bablishi kubwa sana mdomoni ambayo inanitesa sana kuitoa hadi ndoto inaisha iyo bablishi inanata sana kwenye meno na navyoitoa haishi mdomoni hadi nashtuka na meno yanauma sana. Mda mwingne navyoangaika kuitoa nahisi nashindwa kupumua. Kwa mtu anayejua ndoto naomba msaada tafadhali niweze kuepukana na hili.

Kamuone daktari wa kinywa.
 
Kabla ya kulala piga magoti usali,kusali ni kuongea na Mungu,kwahiyo hakikisha wakati unasali mazingira ni masafi na hapo mahali ni tulivu,tubu makosa yako,mueleze shida yako na umuombe akuepushe na hiyo ndoto.Hutaamini utalala usingizi mzuri na huo utakuwa mwisho wa hizo ndoto.
 
Mshana samahani me na ndoto uwa naota mara nyingine natoa manyoya mdomoni ya kuku yaweza kuwa sawa na hiyo? Kama ni sawa na hiyo ntafanyaje kumjua mbaya wangu?

Ni michezo ileile tu dawa yake ni ileile tu
 
kwani hujaweka ulinzi shirikishi kwenye boma lako?
 
Pole sana kijana,nisikuchoshe kwa maelezo marefu ila kuna dalili kubwa kuwa una sumbuliwa na shetani.maana ndoto zipo pande tatu.kuna ndoto za mungu kuna ndoto za kishetani na ndoto za mawazo binafsi.ndoto za mungu huwa zina leta ujumbe fulani maalum,ndoto binafsi huwa zina leta ujumbe kulingana na mawazo yako,na ndoto za shetani huwa za mateso zaidi endapo haumtii na Mara nyingine huwa za maono Fulani endapo una mtii.ndoto za mungu na binafsi si zenye kujirudia kwa wakati mmoja baada ya Sikh maalum Mara kwa mara kwa kufanana mazingira.
 
Hiyo ni michezo ya wanga wanakulisha ngozi za wanyama most likely fisi,cha kufanya lala na mfupa wa kitimoto au pakaza mafuta yake kitandani au ukiweza jipake mwilini wakati wa kulala
wanamlisha wakiwa physically ndani ya nyumba yake ama wanakuwa remote then wanatuma kupitia jina lake?/
 
Kabla ya kulala piga magoti usali,kusali ni kuongea na Mungu,kwahiyo hakikisha wakati unasali mazingira ni masafi na hapo mahali ni tulivu,tubu makosa yako,mueleze shida yako na umuombe akuepushe na hiyo ndoto.Hutaamini utalala usingizi mzuri na huo utakuwa mwisho wa hizo ndoto.
Imani si jambo la lelemama, inatakiwa kujitoa kwa Mungu kabisa kabisa, siyo leo unasali then kesho yake upo bar unalichafua hekalu la bwana!! wanga lazima wataku-beep tu.
 
Inawezekana una tatizo la kusaga meno (bruxism) ukiwa umelala ndio maana ukiamka meno yanakuwa na maumivu, jaribu kumwona daktari.
 
Mshana usiwadanganye watu.Hii ndoto ni michezo ya kichawi anayofanyiwa huyu jamaa.Na kumwambie alale na mifupa au apake mafuta ya nguruwe ni kumdhalilisha tu mwenzio.Shetani hamwogopi nguruwe.Shetani anamwogopa Yesu tu.Kwahiyo jibu la tatizo hili ni kuishi maisha matakatifu ndani ya Yesu ili Shetani asiweze kumchezea.Full stop.
Hiyo ni michezo ya wanga wanakulisha ngozi za wanyama most likely fisi,cha kufanya lala na mfupa wa kitimoto au pakaza mafuta yake kitandani au ukiweza jipake mwilini wakati wa kulala
 
Back
Top Bottom