Naombeni msaada wa kisheria katika hili jambo

Naombeni msaada wa kisheria katika hili jambo

Hiphop

Member
Joined
Jul 17, 2010
Posts
51
Reaction score
7
Mimi ni muathirika wa zoezi la bomoa bomoa ambalo linatarajiwa kufanyika hivi karibuni,ninahitaji ushauri wa kufahamu haki zangu maana tumeambiwa na serikali kama tumevamia eneo hilo kutokana na vipimo vya barabara vilivyo hivyo tunatakiwa kupisha mpango wa barabara wa serikali. Swali langu ni je sisi wakazi wa maeneo hayo ambao tumeishi muda wote bila kupata usumbufu serikalini na maeneo yetu yalipimwa na maafsisa ardhi na baadhi yetu tuna hati na tumeletewa huduma mbali mbali na serikali kama umeme na maji, je hatuna haki ya kuapata fidia yoyote juu ya ardhi?kama status yetu ni ya wavamaizi je maendelezo tuliyoyafanya katika ardhi ile pia hatuwezi kulipwa?Naombeni mnisaidie nijue kama nina haki katika jambo hili.
 
Eminent domain laws come into play in your situation. I will get back to you.
 
Una haki ya kulipwa na kwasababu vithibitish vyote unavyo naamini utalipwa kulingana na sheria ya ardhi inavyoainisha ila wakikuletea longolongo una haki ya kwenda kushtaki mahakamani
 
Nakuhurumia ni jinsi gani unaweza kufanikiwa kuipata haki yako ambayo kimsingi nafkiri unayo katika mahakama zetu zilizolemazwa na urasimu pasina kuwa na mwanasheria. Kwakifupi unaweza kuwa na haki uliopatiwa na katiba, haki ya kumiliki lakini pia yakulipwa fidia inayotosha pale unaponyan'ganywa umiliki kwa manufaa ya UMMA (serikali iko liable kwa acquiescence/ yaani mlipaswa kuzuiwa). Pamoja na yote hayo mnahitaji kumuona mwanasheria makini kwa msaada zaidi, ilikutetea haki zenu. Lakini endapo hauna huwezo unawexza ukaomba msaada toka kwenye asasi za haki za binadamu ikusaidie kushitaki kama maskini (paupa).
 
Mimi ni muathirika wa zoezi la bomoa bomoa ambalo linatarajiwa kufanyika hivi karibuni,ninahitaji ushauri wa kufahamu haki zangu maana tumeambiwa na serikali kama tumevamia eneo hilo kutokana na vipimo vya barabara vilivyo hivyo tunatakiwa kupisha mpango wa barabara wa serikali. Swali langu ni je sisi wakazi wa maeneo hayo ambao tumeishi muda wote bila kupata usumbufu serikalini na maeneo yetu yalipimwa na maafsisa ardhi na baadhi yetu tuna hati na tumeletewa huduma mbali mbali na serikali kama umeme na maji, je hatuna haki ya kuapata fidia yoyote juu ya ardhi?kama status yetu ni ya wavamaizi je maendelezo tuliyoyafanya katika ardhi ile pia hatuwezi kulipwa?Naombeni mnisaidie nijue kama nina haki katika jambo hili.

So long as umepimiwa na ukapewa na hati ( iwe offer au hata title di) ya kumilikishwa ardhi basi kwa mujibu wa sheria za Ardhi za Tanzania utalipwa na kupatiwa kiwanja kingine kama compasation.

Ondoa shaka
 
Back
Top Bottom