Hiphop
Member
- Jul 17, 2010
- 51
- 7
Mimi ni muathirika wa zoezi la bomoa bomoa ambalo linatarajiwa kufanyika hivi karibuni,ninahitaji ushauri wa kufahamu haki zangu maana tumeambiwa na serikali kama tumevamia eneo hilo kutokana na vipimo vya barabara vilivyo hivyo tunatakiwa kupisha mpango wa barabara wa serikali. Swali langu ni je sisi wakazi wa maeneo hayo ambao tumeishi muda wote bila kupata usumbufu serikalini na maeneo yetu yalipimwa na maafsisa ardhi na baadhi yetu tuna hati na tumeletewa huduma mbali mbali na serikali kama umeme na maji, je hatuna haki ya kuapata fidia yoyote juu ya ardhi?kama status yetu ni ya wavamaizi je maendelezo tuliyoyafanya katika ardhi ile pia hatuwezi kulipwa?Naombeni mnisaidie nijue kama nina haki katika jambo hili.