Naombeni msaada wa kisheria na ushauri

Jeff

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2009
Posts
1,293
Reaction score
200
Habarini za Usiku huu wana JF.
Naombeni msaada au ushauri kwa jambo hili.
Nimetumia parccel kutoka nje ya nchi (smartphone 2) kwa EMS, risiti inaonyesha siimu zina gharama ya usd 80 na jamaaa amelipia insurance.
baada ya mzigo kufika bongo posta wakaaniambia niende TRA ili wafanyee hesabu ya kodi ya mzigo, nikaenda TRA nikiwa na risiti ya mzigo inayoonyesha kuna simu 2 na gharama yake ni usd 80. na zimetumwa kama gift.
Sasa TRA wanasema hiyo sio bei halisi ya hizo simu kwa hiyo mahesabu ya kodi wananipigia kwa bei ya simu wanavyojua wao kuwa hizo simu zinaagharimu kiasi gani kwa hapa bongo.
Simu zenyewe ni samsung LT4G, wameniambia nilipe Tsh 190,000/= kwa kila simu. Baada ya kuongea nao na kuwaambia sina hiyo hela wakapunguza mpaka laki moja kwa kila simu. nikawaambia tena sina hiyo hela
Na nimewaambia kuwa ikishindikana bora mzigo urudishwe kwa mtumaji maadam una insurance.
Mimi binafsi nimejiuliza maswali 2
1. kwanini wang'ang'anie bei zao za kitanzania na wakati mzigo umeandikwa thamani yake kwenye risiti na watu wa insurance wamekubai kupokea dhamana ya mzigo huo kwa kiasi cha 500,000
2. Hawajaniweka wazi formula inayotumika kucalculate hiyo kodi ppamoja na VAT
Naombeni msaada wa kisheria na ushauri katika hili tafadhali
 
TRA wakashusha bei kama wafanya biashara duh au mimi ndo sijaelewa mana halmashauri ya kichwa change inahisi haao watakua matapeli
 
TRA wana mamlaka ya kukataa risiti yako ikiwa watakuwa na mashaka ya bei, then wataangalia hapa kwetu hicho kitu kinauzwaje ndo wanakupigia hesabu ya kodi

Ushauri wangu ongea nao wakupunguzie kodi kwani wana mamlaka hayo pia kutegemea na thamani ya kitu chenyewe. Ukisema uende nao kisheria ndo utakwama mazima
 
kulingana na sheria za kodi wataangalia Fair value.. je wakati unanunua hiyo simu relation iliyokuwepo kati yako na muuzaji je ilikuwa business. kama ni business lazima kuwepo na Arm length transaction..
Ref. Internatinal Financial Reporting Standard IFRS 13..
 
Ila kama ni gift wamesema kwa nini wanataka kodi?

Hata mie nashangaa ingekuwa inatoka kwa kampuni uliyonunua sawa wangedai ila kupokea zawadi nashangaa.

Ni sawa kama wanapouliza airport wakiambiwa kitu walichoulizia kuwa ni zawadi hawawezi kudai.

Nchi nyingi zawadi ikija bila kutoka iliponunuliwa ni zawadi no kodi. Kuandika bei ni kawaida kwa sababu ya bima kusafirisha ikitokea ikapotea.

Wanataka kuweka mfukoni, ulizia kipengele chao cja kupokea zawadi kinasemaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…